Mdada mmoja mwenye shughuli za kisanii anayeendesha Pub yake
maeneo ya Kinondoni, siku moja alifunga Pub yake kama saa nane ya usiku, kafika
kwake akiwa hoi, ile usingizi unaanza kumpata simu yake ikalia, sauti ya kilevi
ikasikika;
SAUTI: Hallo mchumba, Pub yako unafungua saa ngapi?...... kwa
hasira akakata simu. Baada ya dakika chache ikalia tena
SAUTI: Hallo we dada, saa ngapi unafungua Pub yako husikii?.
Mdada akakasirika;
MDADA: Sikiliza wewe acha kunisumbua na ujinga wako hata
ningekuwa nimefungua nisingeruhusu mlevi kama wewe kuingia shenzi
SAUTI: Ngoja , mbona unapaniki, nani kakwambia nataka kuingia?
Mi nataka kutoka umenifungia
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE