Jamaa kataarifiwa kuwa kuna mtu anatoka na mkewe, akaamua
kupanga fumanizi kumaliza ubishi. Siku hiyo akapata taarifa kuwa mkewe atakuwa
Ugonelye Guest na jamaa yake, akafanya Umafia wa hali ya juu na kweli akamkuta
mkewe na jamaa wakiwa hoi kwa raha zao. Mgoni akakimbia wakabaki mtu na mkewe.
Jamaa machozi yakawa yanamtoka kwa uchungu;
JAMAA: Mke wangu yaani unanifanya hivi mimi? Unanisaliti
bila huruma, Nimekukosea nini mimi?
MKE: Mume wangu nakiri nimekukosea, najisikia vibaya sana,
kuna kitu naomba niongee
JAMAA: Tena useme kinachoeleweka kabla sijakuuwa, nina
hasira sana.
MKE: Mi nimekukosea mno, kwa hiyo naomba uniache
JAMAA (kwa upole): Ngoja kwanza mbona unafika mbali, mi
sijafika huko
MKE: Hapana mume wangu, we niache nimekudhalilisha sana, mi
naenda kwetu
JAMAA: Sio hivyo mke wangu, tufanye haya ya leo yamekwisha
tuanze ukurasa mpya
MKE: Mi sitakuwa na raha, na ninaweza kukusaliti tena
JAMAA: Usijali hayo mke wangu mi ntakuwa nakusamehe
MKE: Mi naenda nakwenda kwetu
JAMAA: Please please usiende kumbuka tuliko toka, haya ni
mambo madogo……………….kesi inaendelea
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE