Jamaa fulani alikuwa na tabia ya kujamba kwa nguvu
kila aamkapo asubuhi. Mkewe alikerwa sana na tabia hiyo, alimkataza akachoka,
siku moja akamwonya kuwa iko siku badala ya ushuzi, utumbo utakuja kumtoka.
Jamaa alicheka sana kusikia hilo. Siku moja mke alilazimika kuamka alfajiri
awatengeze kuku kwa ajili ya sherehe, alipowatoa utumbo wale kuku akakumbuka
alichowahi kumwambia mumewe akaamua kumtisha, akamnyatia mumewe ambaye alikuwa
bado amelala na kumuwekea utumbo kwenye pajama lake na kurudi jikoni. Muda si
mrefu mwanaume aliamka na kufanya mambo yake kama kawaida, lakini akahisi kitu
cha baridi ndani ya suruali, ile kuvuta si akakuta utumbo. Akapiga
ukelele,’Mama yangu nimekufa’. Mke wake aliposikia akacheka peke yake, akajua
jamaa kashaukuta ule utumbo. Kimya cha kama nusu saa kilipita. Hatimaye jamaa
akamfuata mkewe jikoni akiwa amelowa jasho pajama nzima.
JAMAA: Mke wangu yale uliosema leo yametokea.
MKE: Yepi jamani?
JAMAA: Mke wangu utumbo si umetoka kama ulivyosema
MKE: Pole mume wangu, sasa?
JAMAA: Namshukuru Mungu, nimejitahidi nimeusindilia
na vidole na nimeweza kuurudisha ndani wote.
MKE: Mungu wangu umefanyaje?
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE