Kwa
kipindi sasa kwa niaba ya blog ya www.chekanakitime.blogspot.com
nimekuwa napokea tuhuma nzito kwa njia ya ujumbe kwenye facebook, text message
kupitia namba yangu 0758474500, na baruapepe kupitia jokitime@gmail.com unaonaee. Tuhuma hizi
nzito kutoka kwa watu mbalimbali eti NINA WAVUNJA MBAVU haziwezi kuachiwa
zipite hivi hivi na kuenea kitaifa na kimataifa bila kupingwa kwa nguvu zote na
mimi kama mtuhumiwa mkuu wa kuvunja watu unaonaee.
Mimi
ni mzee mmoja mtanashati, si mrefu wala mfupi, nina tabasamu la wastani, mwendo
wa kudunda japo si sana unaonaee. Nina sura ambayo imepambwa na mustachi
uliyosheni ndevu nyeusi ambazo kwa mbali zimepambwa na mvi chache zilizopangwa
kisayansi na hivyo kuleta mvuto ambao wenye busara huuona toka mbali na kutoa
sifa kitaifa na kimataifa, unaonaee. Wanaonifahamu wananisifia kitaifa na
kimataifa kuwa mimi ni mpole, mtaratibu ambaye hupata majonzi makuu kama
nikimkanyaga hata sisimizi kwa bahati mbaya, wengi wanajua hata kwangu mbu
hupendelea kuishi kwa wingi kwa kujua mimi si mmoja wa wale watu makatili ambao
hudiriki kununua sumu ya mbu na kufukizia
ili kufanya kitendo cha ukatili wa kuuwa kiumbe hiki chenye sauti
nyororo kiitwacho MBU unaonaee. Sasa turudi kwenye tuhuma hizi nzito za mimi
kuvunja watu mbavu, tuhuma hizi ninaweza kuziweka katika makundi makubwa
mawili, wababa na wamama.
Kuna wababa wanalalamika kuwa nawavunja
mbavu, na kuna wamama, ambao wengine singo wengine mered wengine hata
hawajulikani wako kundi gani, maana status za Facebook zao zinabadilika kama
taa za disco, singo, mered, not singo, double he wajameni, ene wei wote hao
wamo katika kunituhumu kuwa nina WAVUNJA MBAVU. Hebu tuangalie kitendo cha kumvunja
mtu mbavu, kwanza ni kitendo kinachohitaji ukatili na nguvu za ziada, maana baada ya kumkumbatia mhusika
na kumkamua kwa nguvu mpaka usikie taaaa, ndio unajua hapo mbavu imevunjika.
Sasa ukirudi kwa wababa,kwanza nakataa tena nakataa sijawahi kumkumbatia mbaba yoyote, hata
kama ni kwa salamu zile za kiuwana siasa unaonaee, na pili sijawahi
kumukumbatia mbaba nikamminya mpaka nikamvunja mbavu, hebu pata picha mi na
mustachi wangu huu wa ukweli, nimembana mbavu mbaba mwenzangu, jamani, this is
scandalous, si vizuri kunituhumu mambo kama hayo jamani. Kuhusu wamama nao hebu imajin napita
maofisini, kamata sekretari bana mbavu mpaka zivunjike, kamata sijui programe
ofisa bana, marketing bana (lakini hawa wa maketing kweli kuna haja ya
kuwavunja mbavu, nawaomba matangazo wanani promise kwa kizungu,’ Yua blog is so
fanii, wi wil kol you tumoro’ ndio jiiii au ndio ile ya tumoro neva kams?)
unaonaee Haya naingia maintanet kef, shika wadada minya mbavu mpaka zivunjike,
jamani walimwengu hamuoni kuwa tuhuma hizi ni wazi si za kweli? DHEAFO KWA HIYO…NATANGAZA
KUANZIA LEO NTWABURUZA MAHAKAMANI WOTE WATAKAO NITUHUMU KUWA NIMEWAVUNJA MBAVU.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE