1 October 2012

MABEIBY WANAVAA KIDIJITALI


Kwa kweli ukweli lazima usemwe, wahenga walisema penye analog badilisha weka dijito unaonaee. Mambo mengi yamebadilika na kuingia katika mfumo wa dijito kabla hata ya wenye dijito wenyewe hawajaruhusu au kushtukia unaonaee. Kwa mfano leo nilikuwa sehemu nikapewa ofa ya lanchi na mbosi mmoja ambaye alikuwa na bodi gadi wake wa kidijitali, sasa utaniuliza bodigadi wa kidijitali alikuwa roboti? No no no no, hapana huyu naweza kulinganisha na TV dijito, zenyewe zinakuwa nyembamba hazina chogo, sasa mabodigadi analogu utawakuta wamenuna, wana gogoz nyeusi ambazo huzivaa hata gizani, vifua vipana vyenye misuli ya kuchana T shirt, lakini mabodigadi dijito, wembamba hao kama huyu wa rafiki yangu wa kampuni ya mambo ya jua pale Ubungo, slim, mcheshi kavaa spektakoz za kupima, lakini ukimgusa bosi wake ndio utajua dijito mana yake nini. Thiz days za dijito, ni vizuri serikali nayo iende na wakati, badala ya mapolisi wenye vitambi mkanda kiunoni, twende kidijito zaidi waruhusiwe askri wembamba wenye kuvalia suruali chini kidogo ya kiuno, waruhusiwe kunyoa kiduku unaonaee, macheni shingoni kwa sanaa au vipi, yaani na sie TZ tuwe waanzilishi wa kitu unaonaee.
Kwa mfano siku hizi wako wadada wengi wameshaanza kuwa na akili za kidijito, yusii sisi wenyewe wababa tukiwa nao karibu utatusikia “Hello Baby” sasa kwa kuwa wana akili za kidijito wameanza kuvaa nguo kama babies, si unajuaga vibebi nguo zao chacheee, nepi tu kabebi kanaona poa sana, tena mazake ndio mwenyewe anaekuwa wa kwanza kukapunguza nguo ili kasidhurike ngozi na joto unaonaee. Kwa hiyo hawa wabebi wakubwa nao wanaenda kidijito wanapunguza nguo taratibu. Kwa kiukweli kwa vile wanaitwa beby wataendelea kuvaa kama vile vibebi vingine unaonaee.  Nimalizie kwa madereva wenye ubongo umejaa pumba za kidijitali, hawa bwana kutokana na wao kuwa na akili kuliko wengine ambao bado akili zao analogi, basi usiwashangae wakiamua kuvuka taa nyekundu bila kujali kitakachotokea, wanawasha taa au kupiga honi tu wanajua itatosha, au udijito wao huwaruhusu kuovateki foleni hata ya magari ishirini kisha wanaenda kukwamisha kila mtu mbele, utaona wanjichekelesha wanapotukanwa matusi ya kianalogi na kujitia kuangalia kwenye kioo kama nyuma kuna askari, kumbe hapo wanaona aibu kiaina unaonaee. Ila kuna hawa madereva wa bodaboda ambao brein zao zinatakiwa zipelekwe nchi za nje zikapimwe maana sio dijito wala analogi, wao wanaamini ukipiga honi tu hatari zote zinapotea unaonaee

No comments:

Post a Comment

SEMA USIKIKE