Mkutano wa mwaka wa dunia wa akina mama walioolewa ulikuwa inaendelea, na akina mama kutoka
nchi mbali mbali walikuwa wanatoa ripoti ya utekelezaji wa maazimio ya mkutano
wa mwaka uliopita;
MAMA UK: Baada ya maazimio ya mkutano wa mwisho kuwa lazima waume
zetu waanze kupika chakula wenyewe, nilipofika London nilimueleza mume wangu.
Siku ya kwanza sikuona kitu, siku ya pili pia sikuona kitu, siku ya tatu
mwenyewe aliingia jikoni na kuanza kupika (Makofi na vigelegele)
MAMA USA: Baada ya maazimio ya mwaka jana niliporudi Washington, nilimwambia
mume wangu kuwa sitampikia wala kumfulia tena. Siku ya kwanza sikuona kitu,
siku ya pili alifua nguo chache, siku ya tatu mwenyewe alifua na kupika (Makofi
vifijo na vigelegele)
MAMA TZ: Baada ya maazimio ya mwaka jana, niliporudi kwetu Musoma,
nikamwambia mume wangu kuanzia leo, lazima ujipikie mwenyewe, ufue nguo zako
mwenyewe, ufagie nyumba na kutandika kitanda mwenyewe. Siku ya kwanza sikuona
kitu, siku ya pili sikuona kitu, siku ya tatu sikuona kitu, siku ya nne kwa
mbali nilianza kuona kwa jicho la kushoto, maana uvimbe usoni ulianza kupungua
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE