Kwa Mzee Roman Abramovich,
Chelsea
Stamford bridge
ULAYA
Shikamoo. Mimi
ni mmoja wa wapenzi wa soka duniani, na kwa muda mrefu nimekuwa
ninafuatilia mambo ya klabu yako yanavyokwenda kiukweli nina masikitiko sana.
Ulipokuja Tanzania nilijua umekuja kutafuta njia ya kusov matatizo ya klabu
yako, inaonekana pengine ulitapeliwa maana huku tuna wataalamu wazuri sana, klabu zetu za hapa hutumia mamilioni kwa
ajili ya wataalamu hawa, na kwa kweli
wataalamu hawa wanasaidia sana sema hawa viongozi wa klabu ndio huwa
wanakiuka masharti, mtu anaambiwa asivuke barabara kwa siku tatu ye akitoka kwa mtaalamu tu anavuka, au mara nyingine wanakataa masharti, kwa mfano juzi wazee flani waliambiwa wachanjwe chale za kiunoni eti wakakataa, sasa klabu itapataje maendeleo kama watu mnakuwa wabishi? Kuna mjomba wangu
mmoja alinambia kwa mfano ungekuja huku angekuchanja wewe chale kwenye nyayo kwa niaba ya
klabu maana wewe ndio nguzo, yaani mwenyewe ungeona maajabu baada ya siku
tatu, wabaya wako wote wangekuja kukuomba msamaha na wote walioiendea vibaya
timu wangeumbuka. Hivi kufukuza makocha mara sijui ya 9 haisaidii kwa kuwa
wabaya wako wamekutupia wewe mkosi halafu hirizi wakatupa kwenye shimo la choo kimoja
huko Uwanja wa Fisi, Manzese…(hii ni sehemu moja kubwa sana huku Dar es Salaam), sasa bila
kuteguliwa hiki kipengele utabadilisha sana makocha. Halafu hapa Dar tunaye
Kocha wa Ulimwengu, hivi juzi tu kaacha bendi yake ungemchukua huyu mtoto wa
Bagamoyo angekusaidia sana kuimarisha timu.
Mkuu halafu timu yako haina mabaunsa hili ni tatizo utakuta
kila mtu anaingia klabu bila ruksa hii inawapa wabaya wako nafasi ya kuja
kumwaga dawa zao kwenye vyumba vya wachezaji, huku kwetu tuna mabaunsa
wanauzoefu wa toka enzi ya Gulamali( huyu alikuwaga Abramovich wa huku).
Sisemi mengi we ukiwa tayari nipigie ntakuunganisha tu huku
kuna waganga wa Kinaijeria, kimasai, wakutoka Sumbawanga, kigoma, yaani wewe tu
Mpenzi wa
Chelsea
0713274747
Anko

No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE