![]() |
| Toka kushoto; Mimi, Bada C Ugali(msemaji mkuu Afrika), Don Othman(mpiga picha), Totoo(mcheza show wa shirika), Waandishi wa Habari, Mstari wa nyuma Wasomaji wa habari |
Waheshimiwa waandishi, waheshimiwa wapiga picha za mnato,
waheshimiwa wapiga picha za video, waheshimiwa makanjanja, waheshimiwa mabibi
na mabwana. Kwanza naomba nichukue nafsi hii kuwaombeni radhi kwa hali iliyopo
hii ni kutokana na kuanguka kwa transfoma moja ambayo watoto wa Uswahilini
waliipiga mawe jana asubuhi. Lakini tatizo hilo linashughulikiwa na mafundi
wetu mahiri.
Leo shirika limenituma nije kuongea na nyinyi ili kuondoa
uvundo, samahani uvumi ulioenea kwenye vyombo vya habari vya ndani, nje na hata
pembeni yetu na pia kwenye mitandao ya kijamii na isiyo ya kijamii kuhusu
utendaji wa shirika letu, na hivyo kuchafua jina tukufu la shirika letu la Ugavi wa Giza. Mnaonaee
Awali ya yote nichukue nafasi hii kumpongeza Rais wetu kwa
kushinda kwa kishindo katika uchaguzi uliopita, pia nichukue nafasi hii
kumpongeza Waziri wetu kwa ukakamavu wa hali ya juu kusimamia mishahara na marupurupu yetu wakati wa Bunge
lililopita. Mheshimiwa Waziri take it from me wafanyakazi wote na wake zao
wanakupenda ile mbaya unaonaeee.
Baada ya hayo nirudi kwenye mada. Katika siku za karibuni
kumetokea kundi la watu wasiopenda maendeleo, wapinzani wa juhudi zetu ambao
wamesimama kidete kulaani na kubeza juhudi zetu za kuimarisha sekta hii ya
giza. Uwongo mkuu wanotumia ni kuwadanganya wananchi wenye nia njema eti kuna
mgao wa giza. Ndugu waandishi nyinyi wenyewe mtakubaliana na mimi baada ya kuwagawieni
mshiko wenu mwisho wa kikao kuwa huu ni uwongo wa wazi. Au siyoooo?
Kinachotokea hapa si mgao hata kidogo, bali ni matatizo ya
kiufundi ambayo yanatokana na sababu mbalimbali, kwa mfano hali tuliyonayo hapa
ni kosa la watoto waliopiga manati transfoma, ikatikisika katika vibration
chamber, jambo lililokoz internal bleeding ya oilcom, hapo kilichotokea ni zile
Read Only Memory kukatika na kusababisha kutrip kwa excel,iliyoangusha transformer na kusababisha
kinachoonekana mgao. Katika sehemu nyinge kweli kumefanyika downloading kubwa
kwenye hizi internet café ambazo zimezagaa bila mpango, sasa kuna vijana
wamedownload gigabyte nyingi mno hivyo kukoz internal hameorage ya system na
kuonekana eti ni mgao. Wananchi wenzangu tuache hi dhana potofu ya kuhisi kitu.
Ukweli ni kuwa mkipunguza kudownload kwenye hizo internet café nchi nzima
haitakuwa na mgao wa giza. Otherwise tutaendelea kulaumiana.
Pia niongelee hili swala la kununua kuni za matumizi ya kampuni yetu
nje ya nchi wakati huku kwetu kuni ziko, jamani this is biznes, na katika bizness, kuna
balance sheet, profit and loss account, kitaalamu balance sheet, msichanganye
hii na bed sheet, ni kitu muhimu sana kuangalia, kwa sababu matokeo yake
yanakuja onekana kwenye profit and loss account. Tujiulize hivi ukijiuzia
mwenyewe , how are you going to balance sheet? Tusiwe wepesi tu kutamka , ni
muhimu kuwa na client wa kutoka nje ambaye kwenye accounts zetu hujulikana kama
external account, ambapo biashara hii inakuwa na sura ya kimataifa zaidi. There
fore kununua kuni nje ni kuimarisha biashara kimataifa zaidi, we are making a
name of ourselves and the Nation. Kampuni inakuwa ni ya kimataifa zaidi. Tushirikiane kwa nguvu zote kutetea kuni za njee, ili zetu nazo ziuzwe nje baada ya kukosa soko la ndani unaonaee. Ndugu waandishi baada ya mkutano huu wote mkachukue kabahasha kadogo ka laki sita sita za nauli ya kuwafikisha kwenye ofisi zenu, tukiwa pamoja nchi itaendelea.
Kauli mbiu yetu ni giza ni mali, bila giza hakuna tochi, bila giza hakuna jenereta, giza hoyeeeeeeeeeeeeeeeee

No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE