Habari zilizonifikia
kutoka kwa mtu mkubwa ambaye ameomba nihifadhi jina lake (ili isijulikane kuwa yeye ndiye mbeya), ni kuwa uongozi wa
mkoa mmoja unaoongoza kwa vituko na ambao uko baharini kabisa na wenye magazeti
mengi kuliko mikoa mingine umeamua kupitisha sheria ndogo ya kusajili wapenzi kabla
ya Valentine day ili kuepuka ngumi na fujo siku hiyo. Kila mwenye mpenzi
atalazimika kwenda kwa ofisa utamaduni na kusajili jina la mpenzi wake .
Taratibu zinafanywa ili teknolojia itumike ambapo ukisajili jina la mtu, sms
inaingia kwenye simu ya yule uliemsajili ili akubali kuwa anakutambua na hapo
usajili unakamilika. Pia kama kisha sajiliwa na mwingine usajili utagoma.
Ushauri wangu ni kuwa kwa kuwa tunafahamiana mambo yetu, wahini kwa maafisa utamaduni kabla hamjawahiwa na wengine.
Anko J Kitime
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE