Si rahisi kujua siku yako ya kifo, lakini kuna watu hupata
bahati ya kujua muda umefika. Hapa ni baadhi ya mambo ambayo yatakusaidia kujua
kuwa saa yako ya kifo imewadia…..
UTAJUA KUWA MUDA UMEFIKA..pale ambapo majambazi wenye silaha wameteka gari lenu wote mkaambiwa mtoe simu zenu na atakaeficha atakatwa panga, wewe ukatoa NOKIA tochi na
kumuhakikishia jambazi kuwa ndio simu unayoitegemea, mara Samsung S4
uliyoificha kwenye chupi ikaanza kulia...............
UTAJUA KUWA
MUDA UMEFIKA pale ambapo unawasha kiberiti kucheki kama kuna mafuta kwenye
jenereta iliyozima ghafla....
UTAJUA KUWA MUDA UMEFIKA pale mpenzi wako anapokwambia,
“Ingia uvunguni mwa kitanda mume/mke wangu kaja”. Wakati uko uvunguni simu yako
ya Mchina inaanza kuita.........
UTAJUA KUWA MUDA UMEFIKA pale dreva wa bodaboda uliopanda anaipigia honi treni impishe kwenye kivuko
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE