KAZI KAZI KAZI JOB JOBLESS...Blog yako mzigo ya www.chekanakitime.blogspot.com mwaka 2014 itaanza kwa kutoa taarifa mbalimbali za mambo yanayotokea na
yasiyotokea hapa nchini na hata kote duniani na ulimwenguni. Ili
kufanikisha azma hiyo kunahitajika waandishi wasio mahiri na waliofeli
kozi za uandishi. Hii inatokana na kuwa wale waandishi waliopata bahati
ya kupasi tunaona kila siku kazi zao katika
vyombo vyetu vya habari, sasa tungetaka kutoa nafasi kwa wale waliopata
nafasi ya kufeli ili nao tuone umahiri wao uliosababisha wakaweza
kufeli. Kazi hii ambayo haitakuwa na mshahara ili tuwe tofauti zaidi na
hawa waliopasi inaanza mara moja, kazi kwako ni kuni inbox maombi ya kazi
unashauriwa usitaje jina lako la ukweli ohhooo, stori nyingine ukileta
zinaweza kusababisha ukong'otwe mtaani kwenu au ulogwe na wasanii au
Wakurugenzi wa mashirika unayotaka kuwaumbua, hivyo hapa tuambia aka yako tu. Haya kazi kwenu vilaza.
Kama Mama K anavyosemaga Equal Opportunity For All, hapo najua kingleza kimetowa
kapa tafsiri yake ni hata mafala wapewe chansi
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE