Kila
mtu anapenda watoto wachanga. Hata jitu ambalo huwa mara nyingi halicheki na
mtu liko siriaz wakati wote likikutana na katoto kachanga utakuta linaanza
kutabasamu, tena likibeba katoto kachanga utaona nalo linageuka kuwa litoto.
Utaona linaanza kuongea na mtoto mchanga lugha za ajabu kabisa utadhani
wanaelewana, utasikia, ‘Shum Babu toto shum babu, au shum bibi, shum antii
aijigijigijigi, awawawawa, abububujijiji’ na maneno mengine yasiyoeleweka eti
ndio mtoto atacheka. Leo niwape siri, mnajua kwanini vitoto huwa vinacheka sana?
Vitoto vichanga huwa vinacheka kuona baba zima au mama zima halijui kuongea
vizuri, kitoto kinajisemea moyoni, ‘Huyu mkubwa mzima mzima badala ya kuongea
mambo ya maana eti anasema abujibujibujibuji’ kimsingi watoto wachanga
wanawacheka sana, muwe mnaongea nao kikawaida, sawa ndugu zangu?
Leo
niwape ushauri wababa wenzangu kuhusu taratibu mbalimbali za kufwata kabala ya kucheza na watoto wachanga,
vitoto vichanga vina akili sana
hivyo basi sio kuanza kuvibeba kabla ya kujitayarisha. Najua wabishi
wameshakaa mkao wa kubisha, lazima saa hizi wanasema kimoyomoyo,’ Hakuna kitu
kama hicho, watoto ni malaika’. Mi nasema sawa hebu nisikilizeni kwanza. Wababa
wenzangu, sharti la kwanza usicheze na mtoto mchanga ambaye ndio kwanza katoka
kunyonya wakati umevaa shati la au koti lako la bei mbaya, hakikisha imeshapita
japo nusu saa tangu amenyonya ndipo uanze kumrusharusha. Watoto hawa wajanja
sana, wakijua kuwa umevaa kitu cha bei mbaya watakutaim na kutumia nafasi hiyo kukucheulia maziwa na kama
hukujiangalia vizuri unaweza ukaingia kwenye daladala na michirizi ya maziwa ya mgando mgongoni.
Sharti
la pili linahusu wale ambao hupenda kucheza na watoto kwa kuwanyanyua juu ya
vichwa yao, kabla hujaanza kamchezo hako, hakikisha mtoto kavaa nepi. Katoto
kakijua una kamchezo hako, katajifanya kanacheka sana na kufurahi kila
ukikanyanyua juu, kumbe huo mtego, iko siku ukikanyanyua juu kama hakana nepi
katakutaimu na kukukuharishia kichwani, chunga sana, maana inawezekana wakati
huo mdomo wako uko wazi. Hutu tutoto twa siku hizi tunaanzaga ukorofi tumboni.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE