Jamaa kamkuta mwanamke mmoja pale Ferry analia,
JAMAA: Nini shida mama angu?
MDADA:Heri nife,maisha yamenishinda
MJAMAA: Huna haja ya kufa, sikiliza mimi ni baharia na meli
yetu inaenda Ulaya leo, kama unataka ingia kwenye boksi nikakufiche stoo, meli
ikitia nanga Ugiriki, nakutoa ukatafute maisha huko. Bibie akaona heri hilo
akaingia kwenye boksi, jamaa akambeba na mdada akajikuta yuko kwenye stoo moja
wapo katika meli, jamaa akawa anamletea chakula kila siku na mara nyingine yeye
mwenyewe analala huko kwenye hako kastoo,kila mara akimhakikishia mdada kuwa
wameshapita visiwa vya Komoro, siku nyingine akimwambia wako India. Zilipita
wiki mbili ndipo yule mdada akagundulika na nahodha wa chombo hicho.
NAHODHA:We unafanya nini humu?
MDADA:Chonde naomba msinitupe baharini, nilindeni mkifika
Ugiriki mnishushe
NAHODHA: Unajua mbona sikuelewi? Mdada akalazimika kumueleza
nahodha ishu nzima.
NAHODHA:Dah wala usipate taabu sikutupi popote, ila jamaa
yako kakudanganya hii si meli ya kwenda Ulaya ni pantoni ya kwenda Kigamboni,
tukifika huko shuka
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE