Baada ya kuhangaika muda mreeefu kutafuta njia ya kuingia
studio kurekodi nyimbo zake , hatimae jamaa yangu jina nalihifadhi, akakutana
na jamaa wakamwambia kuwa wao
wanamfahamu mtu mwenye studio. Ndugu yangu akasindikizana na rafiki zake wapya
mpaka jengo moja akaambiwa hapo ni studio, akakuta vijana wenzie nje ya lile
jingo, wengine akawafahamu, wasanii maarufu ambao aliwahi kuwaona tu kwenye TV
na magazeti , hapo akajua lazima nae sasa atakuwa mmoja wa wasanii maarufu
Bongo hii. Baada ya hapo kila siku
akawa anafika pale studio akibembeleza nae kuingia kurekodi wimbo wake, kitu
alichokigundua mapema ni kuwa wengi wa wasanii walikuwa wakivuta sigara, lakini
kichwani akajua hii si sigara halali maana harufu ya sigara hiyo ulikuwa
tofauti, na uvutaji wake uikuwa wa kisirisiri. Baada ya hapo ilionekana waliovuta walikuwa wakichangamka na kuchekacheka bila mpango huku mistari
ikianza kuwatoka mfululizo. Ikaonekana kila mtu anajisifia alivyovuta sigara
hiyo mara ya mwisho mara ya mwisho kwa stori za kufurahisha, jamaa yangu peke
yake akawa hana stori ya kueleza, polepole akaanza kuwaza namna ya kuaanza
kuvuta sigara wanayovuta wale
masupasta. Hilo lilikuwa kosa la kwanza. Swali likawa atapata wapi, na hakutaka
aulize maana wenzie wangejua kuwa yeye mshamba na kuwa hajawahi kuvuta ile sigara wala hajui inapatikana wapi.
Hatimae akagundua kuwa kuna jamaa alikuwa akija pale studio ndio aliyekuwa
akileta zile sigara zenye harufu tofauti. Siku hiyo akamfwatilia na
kumsimamisha. Kwa wasiwasi akaanza, ‘Mambo bro”. Jamaa akajibu, “Poa nikusaidie
nini?” ‘ Nilikuwa nataka ile kitu”. “Kitu gani kuwa muwazi” Hapo akasita maana
hakujua sigara zile zinanunuliwa kwa pakiti au moja moja. “Naomba zile sigara”
Muuzaji akamuangalia machoni,”We mgeni ehh? Haya unataka kiasi gani, aina gani?”,
“Nichagulie wewe ile unayoona nzuri“, Muuzaji akachekaa sana
“Haya leta alfu mbili nikupe kitu cha Makambako chenye mix” ,pamoja na
kuwa alikuwa haelewi maana ya maelezo hayo akajikakamua na kujibu, “Yah hiyo
sio mbaya”. Jamaa yangu akatoa pesa akapewa kitu kimefungwa kwenye karatasi, kwa
spidi akaondoka na kurudi studio. Kufika studio akazunguka nyuma ya jingo ambako ndiko wavutaji
walikuwa wakijificha na kuvuta. Akafungua na kukuta majani haraka kwa kuangalia
wengine akasokota sigara yake na
kuomba kibiriti na kuanza kuvuta. Kosa la pili alivuta moshi mwingi mno,
akaanza kukohoa bila kupumzika, huku wenzie jirani wakimcheka bila kumsaidia.
Akajikaza na kuendelea kuvuta hadi sigara ikaisha, kilichomsikitisha ni
kutokusikia mabadiliko yoyote, na hivyo kujua kuwa katapeliwa kauziwa mchicha.
Haraka akaanza kulalamika kwa wote waliokuwepo pale, “Unajua jamaa kaniuzia
mchicha? Unajua nimeuziwa mchicha?” Kila mtu akaanza kumuangalia kwa makini na
kumshangaa kuhusu mada hiyo mpaya ambayio aliianza ghafla. Jamaa yangu akaingia
studio na kukuta kazi ya kurekodi inaendelea, bila wasi wasi akamtaarifu
producer tatizo lake. “Producer subiri kwanza unajua jamaa kaniuzia mchicha
shilingi alfu mbili” Producer akabaki anashangaa na kumshauri jamaa atoke nje
ya studio. Jamaa yangu huku akishangaa kwanini watu hawamuelewi kuwa alitegemea
kauziwa kitu cha kumpa stimu badala yake kauziwa mchicha. Rafiki zake waliomkaribisha studio
wakamfuata na kujaribu kuelewa nini kinaendelea. Ndipo akawapa mkasa mzima na
kuwaeleza jinsi alivyotapeliwa kwa kuuziwa mchicha kidogo kwa shilingi alfu
mbili. Hapo ndipo wenzie wote wakajua kuwa mwenzao akili si yake. Wakamshauri
apumzike kwenye kochi aondoe uchovu..
Jamaa yangu akawa anasikia sauti kichwani mwake ikimwambia vua nguo kabla hujalala kwenye kochi maana kuna
joto. Hapo akaomba ushauri kwa wenzie avue au asivue. Zogo kubwa likaanza
studio, jamaa yangu akisisitiza kuwa lazima avue nguo ili aweze kulala kwa
amani kwenye kochi. Hapo kazi ikawa kuwaza namna ya kumsaidia jamaa akili
imrudie, wengine wakasema apewe maziwa wengine amwagiwe maji, wengine wakidai
awekwe chini ya feni, mwenye aking’ang’ania kuvua nguo. Ghafla akaanza kudai moyo unataka
kutoka, akawa ajiziba mdomo akidai moyo unataka kutokea mdomoni, na akaatimua
mbio masupastaa kadhaa wakimfukuza. Jamaa akaaingia hoteli ya jirani na kuomba
maji maana moyo unataka kumtoka. Hatimae alikamatwa na wenzie kumrudisha kwao
ambako alikimbilia kwa baba yake na kushtaki kuwa kauziwa machicha wa shilingi alfu mbili na tapeli.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE