Yaani kuna mdada kanitumia barua juzi
anataka ushauri nimebaki nimeduwaa sina la kusema kabisa. Ninachoweza kusema ni
kuwa sasa nina uhakika wa ule msemo wa wahenga kuwa Kupenda Upofu. Hebu na nyinyi hebu someni wenyewe mi nakaa
pembeni.
Anko Shikamoo,
Vipi mzima? Anko mie huwa napenda sana kusoma makala zako,
na zinanifurahisha sana, na nikisoma naona kuwa wewe una busara sana, sasa
nimepata tatizo naomba unipe ushauri babu yangu. Naomba unisaidie pliz. Anko huu
ni mwezi wa nne toka nimeolewa, yaani tayari najilaumu sana kuhusu ndoa hii. Kiukweli
najuta sana. Kabla ya kunioa mume wangu alikuwa anakuja kwangu kila siku na
gari jingine, akanambia kazi yake ni dalali wa magari, na akaniahidi kuwa na
mimi ataninunulia gari ili nisiwe na tatizo la usafiri. Niliongeza mapenzi
kwake ili asijekusahau kunipa gari. Uchumba wetu ulichukua miezi mitatu kisha
tukaoana katika ndoa ambayo mpenzi wangu alisema tufanye kakitu kadogo tu
kakisiri tusiharibu pesa. Ndugu zangu walininunia lakini mimi sikujali. Kwa
kuwa nilikuwa na chumba kizuri katikati ya mji, ilionekana maisha tuanze kwetu
maana mume wangu akisema alikuwa akiishi na mama yake nje ya mji, aliyekuwa
akimkataza asipange chumba. Huwezi kuamini Anko, si juzijuzi tu ndio nimegundua
kumbe nilikuwa nadanganywa siku zote, kumbe mume wangu kazi yake ni kuosha
magari, hana udalali wala nini. Kuna kijiwe chao kando yam to wanaosha magari
mchana kutwa sasa akiachiwa aoshe gari basi ndio huzunguka nalo na ndipo
alipoweza kunidanganya nikaingia kingi. Kwanini alinidanganya vile? Si
angenieleza tu ukweli nijue? Ntaendeleaje kumuamini sasa? Mbaya zaidi mi
nimemaliza chuo kikuu na nimegundua kuwa jamaa hakumaliza hata fom tu, Anko what
do I do? Wenzangu walikuwa wananicheka nilikuwa siwaelewi. Nilikuwa kila siku napiga
picha niko kwenye gari tofauti nazituma instagram, jamani watu wakigundua si
ndio watanichamba mwaka mzima? Ndugu zangu walinionya kuwa wanamuona jamaa tapeli nikagombana nao
sana, narudije kwetu? Anko nipe ushauri.
Hata mimi sijui nimwambieje huyu mdada, hivi alikuwa
fala kiasi gani hakuona kuwa anatapeliwa?
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE