Dogo kampigia simu baba yake;
DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa
nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti
BABA: Unasema nini we mpumbavu mshenzi mkubwa? Nimekukanya
mara ngapi kuhusu kubeti?
DOGO: Lakini baba
BABA: Lakini baba nini ngoja urudi utaona ntakachofanya.
DOGO: Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda shilingi milioni 3
BABA: Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu sana kwanini
hukutumia laki nzima kubeti? Si ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi
niwataarifu ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua haraka mwanangu mpenzi...
pitia www.johnkitime.co.tz
pitia www.johnkitime.co.tz
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE