Wachawi
bado wapo bize sana kama hujui. Halafu wachawi bwana watu wana roho mbaya sana,
ishu zao huwashughulikia watu wao wa karibu tu. Ukiwa mnatoka kijiji kimoja, au
mtaa mmoja au nyumba moja, au nduguyo au rafiki yako, kati ya hao ndo atatoka
atakae kuloga. Kama hakujui mchawi hana shida na wewe. Unajua wachawi wana
mbinu mbaya sana kwa mfano umepiga dili limetiki una tumilioni kadhaa, au
umepokea fedha zako za mafao ya kustaafu, au singo yako imehit, unapitapita kwa
nduguzo au marafiki kuulizia ufanye mradi gani, basi mmoja wapo kama mchawi
atakupa wazo, kwa mdomo au kimawazo, ohh fungua genge au fungua kigrosari, nunua
gari au kalime. Basi utaona bonge la wazo, mihela yako yote unaingiza kwenye
mradi. Kama genge ndio utaona watu wanalikwepa tu, mpaka mtaji unakuishia
hivihivi laiv, kama ulifungua kigrosary utajikuta au wewe mwenyewe unageuka
mlevi unajikopesha hizo pombe na kununulia wateja wako mpaka kamradi kana buma,
kama umenunua kagari, siku mbili tu kamepigwa mzinga, ukijidai kulima basi
mwaka huo ndio bei ya ulicholima kinashuka bei ghafla unaambulia patupu, hapo
ujue kuna mkono wa mtu. Jana na mimi yamenikuta nimelogwa hivihivi najiona. Niliamka
nikiwa na alfu tu, njaa inauma, nikangia kwa mama ntilie nipate japo kikombe
cha chai cha mia, maandazi mawili ya mia na bakuli la maharage la mia tatu.
Hapo nikajua nabakiwa na mia tano, itatosha nauli ya daladala kwenda kariakoo
nikabahatishe chochote. Mama
ntilie akaniletea oda yangu nikaanza kula taratibu, hee kutizama chini hivi si
nikaona mtu kadondosha noti ya alfu, basi kwa ustadi mkubwa nikaivuta kwa mguu
bila mtu yoyote kunishtukia kisha nikaikanyaga vizuri. Roho yangu ikawa sasa na
amani, nilipomaliza raundi ya kwanza nikaagiza tena chai nyingine, maandazi na
maharage. Wakati wa kulipa nikainama na kuchukua ile alfu na kumpa mama ntilie
tukaagana kwa furaha tumbo limejaa safii. Nikakimbilia daladala la Kariakoo
nikakaa tena kwenye dirisha nipate upepo. Mchezo ukanigeukia konda alipotaka
nauli, nilijisachi mwili mzima siioni alfu yangu, machozi yalinilengalenga
nilijua konda hatanielewa. Na hapo ndipo akili ikanijia kuwa ile alfu nilidhani
kadondosha mtu mwingine nilikuwa nimedondosha mimi mwenyewe. Nikagundua mara
moja lazima kuna mchawi kaniroga, na nina shaka na kale kazee mtaani kwetu
nilikokaambia siji kukaamkia dahh kweli uchawi upo
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE