The
Human Resource Manager,
KUBOMA MIKUSU LTD Co.
IRINGA
7 Dec, 2016
KUBOMA MIKUSU LTD Co.
IRINGA
7 Dec, 2016
Mheshimiwa,
YAH: KUKATAA MAOMBI YANGU YA KAZI
Mheshimiwa nakiri kupokea barua yako ya tarehe 3 Novemba 2016, ambayo ulinitaarifu kuwa maombi yangu ya kazi yamekataliwa. Naomba nikutaarifu kuwa sikubaliani kabisa na yaliyoandikwa katika barua yako ya kunikatalia kazi kwenye kampuni yako. Wewe ni HR wa saba kuniandikia barua ya namna hiyo, sasa nimechoka, mmeona kila mkijibu hivyo nanyamaza tu mnaona mi ni mnyonge sana sasa nasema nimechoka. Kwa maandishi yako mwenyewe umekiri kuwa vyeti vyangu ni vizuri sasa tatizo liko wapi?
Kwa hiyo pamoja na sifa kubwa ya kampuni yako, na uzoefu unaouonyesha wa kukataa kuajiri watu, nimeona naikataa barua uliyoniandikia na kwa taarifa yako tafadhali tayarisha kiti na meza yangu, kwani Jumatatu tarehe 12 Desemba nakuja kuanza kazi. Nategemea ushirikiano mwema toka kwako na viongozi wengine
Mi
si mtu wa mchezo mchezo
Ndimi
mtiifu
John Mnyalu
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE