Haya tena taarifa ya Umoja wa Mataifa ndio imetoka na Norway
ndio nchi yenye furaha nyingi kuliko zote duniani. Kwa miaka miwili iliyopita
Norway ilikuwa ya nne na Denmark ilikuwa ya kwanza, mwaka huu Norway imekuwa ya
kwanza. Mwaka huu nchi ya pili imekuwa Denmark, ikifuatiwa na Iceland, Switzerland, Finland, Netherlands, Canada,
New Zealand. Nchi za Australia na Sweden kwa pamoja zimekuwa za tisa. Kwa mwaka huu Marekani ya
14, Ujerumani ya 16, Uingereza ikichukua nafasi ya 19. Urusi ni ya 49, Japan ya
51 wakati China ni ya 79. Nchi ya Rwanda ni ya 151, Syria ya 152, Tanzania ya
153, Burundi ya 154, nay a mwisho ni Central Afrika Republic. Kati ya mambo yaliyopimwa
yalikuwa ni afya, kuwa na mtu wa kumtegemea, uhuru wa kuamua cha kufanya
maishani, uhuru wa kutoka na janga la rushwa
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE