Hahahahaha
kazi kwelikweli, juzijuzi kazini kwetu kulitangazwa semina ya siku moja ya wanaume
waliooa. Kuna taasisi inayohusika na jinsi ya kuendeleza familia zenye Amani,
ilifika kazini kwetu na kututangazia kuwa wanaume wote walio katika ndoa
wahudhurie semina bila kukosa, bosi wetu
akajitolea kulipia chai na chakula cha mchana. Hii ishu sikutaka inipite,
kwanza nilikuwa na maswali mengi sana nilitaka kujua jinsi ya kurudisha penzi
la awali na mke wangu, nilitaka mambo yarudie enzi zile ambapo kila niliporudi
nyumbani nilikuta katandika kitanda vizuri na juu yake kaweka maua. Nilikuwa
nakuta chakula kimefunikwa kawa lenye maneno matamu ya mahaba. Nikitoka kidogo
hata kama nilienda mtaa wa pili kucheza bao, nikirudi namkuta waif kabadili
nguo ananikaribisha utadhani nilisafiri wiki. Nilikuwa natamani enzi zile
zirudi tena
Basi semina
ilianza kwa maelezo mengi na mifano
mingi sana. Mchana baada ya kula, kila mtu aliambiwa amtumie mkewe meseji
kwenye simu. Meseji rahisi tu, aandike neno NAKUPENDA na kulituma kwa mkewe.
Basi kila mtu akaandika na kutuma, baada ya hapo tukaambiwa kila mtu ampe
jirani yake simu yake. Haikuchukua muda mrefu milio ya mesej za majibu zikaanza
kusikika , watu wote tulikuwa kimya. Kisha muwezeshaji wa semina ile akaomba
walioshika simu waanze kusoma majibu yaliyorudi kwenye simu. Ngoma ilianza hapo.
Simu ya kwanza ilisomwa jibu lilikuwa, ‘Vipi baba Jeni, kuna nini?’.
Iliyofuata,’Labda enzi hizo siyo sasa’, nyingine ikajibu, ‘Sikukopeshi tena
huwa hurudishi hela zangu’, nyingine ikarudi imeaandikwa, ‘Umefanya nini tena?
Safari hii sikusamehe?’ Tulianza kucheka sasa, ikasomwa meseji nyingine mke
akajibu,’Sijakuelewa’. Nyingine ikajibu,’Ni wimbo mpya wa Diamond?’, mke wangu
nae akajibu, ‘Usiponambia meseji hii ilikuwa inaenda kwa nani, usirudi’.
Mwenzangu mmoja akapata swali,’Nani mwenzangu?’ Bosi wetu nae alipata jibu toka
kwa mkewe, lilikuwa onyo, ‘Sinilikwambia uache kulewa mchana mume wangu’. Ila
kulikuwa na meseji moja ya jamaa yetu wa uhasibu ambaye mnoko sana wakati wa
kutulipa mafao yetu, ila tulimuonea huruma alipoanza kutoa machozi kutokana na
jibu la mkewe ambaye inaonekana alijichanganya na kujibu,’We vipi nilikwambia
usiwe unanitumia meseji za hivi mume wangu akiziona itakuwa shida’ Na simu ya afisa utumishi ilikuwa na swali, ‘Vipi umemjaza mimba mtumishi
mwingine?’. Tumetoka kwenye semina tumechanginyikiwa kuliko tulivyoingia.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE