BINTI mmoja alisahau simu yake supamaket. Meneja wa supa maketi aliangalia kwenye phone book na kukuta namba imeandikwa 'Mama'. Akapiaga na mama akapokea;
MENEJA: Shkamoo mama mwanao kwa bahati mbaya amesahau simu yake hapa supamaket, unaweza kumtaarifu aje aichukue?
MAMA: Marahaba mwanangu, hakuna tabu na asante sana, nitamtaarifu sasa hivi.
Baada ya sekunde chache simu ikaanza kuita, jina lililotokea ni 'Mama', meneja akapokea na kabla hajajibu mama akaanza kuonea
MAMA: We Fulo, angalia ujinga wako sasa, simu umeenda kuiacha supamaketi, haya nenda ukaichukue sasa hivi usirudi bila simu.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE