Nimewaza sana kuhusu madereva wa bongo, yaani kila nikiwaza najikuta jibu ni moja tu, madereva wa siku hizi ni tofauti sana na enzi zetu. Enzi zetu barabara zilikuwa nyembamba, magari machache tena sio mazuri kama siku hizi, ilikuwa kawaida sana kusikia ajali imetokea kwa kuwa steringi imekatika, au tairi limechomoka, mara nyingine utasikia breki zimefeli. Lakini siku hizi magari yameboreshwa, si rahisi kusikia eti steringi ilichomoka au breki zimefeli lakini ajali ndio zimeongezeka sana. Enzi zetu pikipiki pia zilikuwa za kizamani hazina indiketa, pikipiki zilikuwa na breki za waya ambazo uliweza kusikia zimekatika wakati wowote. Pamoja na hali hiyo ajali za kizembe zilikuwa chache sana.
Sasa siku hizi kama nilivyosema gari zimeboreshwa, pikipiki zimeboreshwa, barabara zimeboreshwa sasa eti madereva nao wameboresha ajali. Madereva wa bodaboda wakiona ajali haziwatokei huamua kuvuka taa nyekundu bila kuangalia kushoto wala kulia. Madereva wa magari nao wakiona siku nyingi hawajapata ajali wanaanza kutuma meseji wakati wanaendesha gari. Sio ajabu ukasikia dreva wa basi aliovateki kwenye kona akiwa spidi kali. Sasa naomba nitoe ushauri kwa serikali. Nimefanya utafiti wa siri nyumbani kwangu, nimegundua kuwa kuna madreva wanakuwa wana ajenda ya siri wawapo barabani. Yaani jama unamuona freshi kabisa anaongea na wewe anacheka kumbe ndani anampango wa kujiua. Au siku hiyo ana hamu ya kuuwa mtu. Dreva akitaka kujiua utaona anachukua simu na kuanza kuchati kwenye simu huku anaendeesha, hapo ujue anatafuta taimingi abamizwe afe. Kama ni dreva wa bodaboda au bajaji, utamuona anajipitisha katikati ya magari kwa spidi moyoni anaomba abamizwe afe. Sasa kuna ule wakati dereva anakuwa na hamu ya kuuwa mtu, hapo ndipo ataanza vituko hivyohivyo huku akiwa na abiria, hapo anajua akikosa kumuua abiria basi atampata mtembeea kwa miguu. Sasa baada ya utafiti huu, nashauri trafiki mkimkamata dreva anavunja sheria barabarani sio mnamtwanga faini, haisaidii, mchukueni kwanza mkampime mkojo kama kavuta bangi, kisha mpelekeni kitengo cha kupima akili, ndipo ijulikane adhabu stahiki. Mi nina akili sana mjue.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE