KUNA mdada nilikuwa nimemuuzia simu, akalipa nusu, hiyo nusu
iliyobaki ikawa tabu kulipa baadae kila nikipiga simu hapokei. Nikaona
nimuandikie meseji,
‘Aise sikuwa na kudai, nilitaka kukwambia nilikuwa napita huku Sinza mori nikamkuta msichana mmoja ambaye boyfriend wako
alimnunuliaga simu toka kwangu anapigana
na mwenzie, eti wanamgombea bwana wako.
Huyu aliyenunuliwa simu kakong’otwa akakimbilia kwenye gari la boyfriend wako
wakasepa’. Haikupita nusu dakika simu ikaanza kuita sikupokea. Baada ya missed
call 13, ikaingia meseji, ‘’Wamepigania wapi? Halafu walielekea wapi? Nambie
tafadhali tafadhali hapa nataka kufa”. Nikaminya nywiiii shenz taip. Ikaja meseji
nyingine, ‘Hela zako ninazo tukutane wapi nikupe unihadithie?’ Nikajibu nitumie
kwa eatel mane, niite uber nikupitie nikupeleke anakokaa huyo mdada, mie napajua'. Nusu dakika baadae mkwanja ukaingia, nikazima simu. Mpaka sasa nimelala feni linanipuliza
taratibu.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE