30 June 2012

Haiwezi kuwaka hii

Maprofesa kadhaa wa chuo cha ufundi walikaribishwa katika uzinduzi wa ndege mpya, wakakaribishwa kwenye viti vya ndege wakafunga na mikanda. Walipopewa maelezo kuwa ndege hiyo ni matokeo ya project ya wanafunzi wao wenyewe, maprofesa wote walitimka nje kabla ndege hata haijawashwa, kasoro mmoja tu akabaki kwenye kiti;
MWANDISHI: Mzee wenzio wote wamekimbia mara baada ya kuelezwa kuwa ndege hii imeundwa na wanafunzi wenu, sasa wewe haukukimbia kwanini Mzee?
PROFESA: Sikuona sababu ya kukimbia kwa kuwa kama imeundwa na wanafunzi wetu sidhani hata kama inaweza kuwaka

No comments:

Post a Comment

SEMA USIKIKE