5 July 2012

2+2=5

MWALIMU:(Akiwa anajaribu kumfundisha mtoto wa darasa la kwanza hesabu) Nikiwa na mbwa wawili halafu nikakupa wengine wawili utakuwa na mbwa wangapi?
KADOGOO: ntakuwa na mbwa watano
MWALIMU : Jamani sijawahi kuona mtoto mjinga kama wewe. Haya nikiwa na mbwa mmoja nikakupa, halafu nikakupa tena mbwa mwingine, utakuwa na mbwa wangapi?
KADOGOO: Watatu
MWALIMU: Pumbavu mkubwa sema wawili.
KADOGOO: Hapana mwalimu watakuwa watatu, sababu nyumbani tayari nina mbwa mmoja.

No comments:

Post a Comment

SEMA USIKIKE