5 July 2012

Baba nimevunja Amoeba ya shule

Baba yangu mpendwa, Shikamoo.
Nakuandikia barua hii nikitegemea kuwa wote hapo  nyumbani mko salama. Je, Uliweza kuuza ng'ombe yule safari hii? Nimengojea sana uniambie kuhusu hilo. Je, mama anaendeleaje?
Nia na madhumuni ya barua hii ni kukutaarifu kuwa huku shuleni mimi nimepata tatizo kubwa ambalo linaweza kuleta matatizo mpaka hata wewe ukafungwa. Baba yangu mpendwa tulikuwa katika shughuli za kawaida tu kwa bahati mbaya nikaangusha chupa iliyokuwa na AMOEBA ndani yake, sasa wanataka kunifukuza shule, au kuja kukukamata wewe mzazi wangu kama sitalipia Amoeba hii ya shule. Shule nzima kulikuwa na amoeba moja tu, maana nyingine zilichukuliwa na serikali siku Rais alipokuja kutembelea shule yetu. Sasa wakimwambia Rais kuwa ukoo wetu ndio umevunja Amoeba iliyobaki ikatuwa hatari sana kwetu. Naomba tafadhali tuma upesi hela kiasi cha shilingi Laki tano ili shule iweze kuagiza Amoeba nyingine kabla Rais hajajua.

Mwanao mpendwa Frank

No comments:

Post a Comment

SEMA USIKIKE