Ni
wazi teknolojia inagusa utendaji wa majukumu ya kila mtu, na kila kitu.
Nimelazimika kutoa tamko hili baada ya kuona mambo kadhaa yanajitokeza ambayo,
awali yalionekana kama hayatakuja kuyumbishwa na teknolojia lakini sasa ni wazi
teknolojia imechukua mkondo wake. Katika kipindi cha miezi michache iliyopita,
nimeweza kusoma hadithi zilizodaiwa kuwa ni za kweli kutoka magazeti yangu
pendwa nisiyokubali kuyakosa kila siku ‘aka’ magazeti ya makolokocho, kuwa watu
wameanza kuwasiliana moja kwa moja kwa njia ya text message, aka ‘kuchati’ na
vitu ambavyo zamani ilihitajika kafala, na wazee maalum, taratibu maalumu tena
katika maeneo maalumu ili kuweza kuwasiliana, na hata hapo ilihitaji watu
maalumu kutafsiri mawasiliano hayo. Kwa maneno mengine watu wameanza kuwasiliana
na majini direct kwa text message. Juzi nimesoma mdada ambaye aliaanza kuchat
na jini, mpaka akatokea kumpenda na mpaka wakapanga wakutane gesti, na huko
walikutana ila jinni alipoingia bafuni kuoga akatoka ameoza upande mmoja!!!!!!,
sasa haya ni mendeleo makubwa sana kiteknolojia, kuwa hata majini wamekubali
yaishe na kukubali kutumia mitandao yetu pendwa, najiuliza tu kama pia
wameshasajili namba zao?
Zamani
tuliambiwa majini walikuwa wanaogopa nguruwe, jana tu katika kijiwe kimoja
nilipewa taarifa kuwa majini hawaogopi tena kitimoto wameshapata anti virus
yake, hivyo kula KITIMOTO si kinga ya majini.
Pia
swala la majini kuogopa bangi nalo linaoneana lina utata, kwani kuna rafiki
yangu mmoja baada ya kuvuta bangi ndipo alipoanza kulalamika kuwa kuna jinni mahaba
linamtaka.
Swali je, kutokana na taarifa hii unauhakika
gani kuwa rafiki zako wote wa Facebook ni binadamu?
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE