Siku ya kufunga shule mzazi
mmoja kaenda na mwanae shule, sherehe zikaanza wanafunzi wakawa wanapewa vyeti
na zawadi kadri ya ubora wa mambo yao, mtoto wa jamaa yetu hakutajwa hata jina.
Mzazi akawaangalia wale watoto waliofanya vizuri akamwambia mwanae;
Baba: Wale ndio watoto,
mbona Mungu kaninyima? Wakaondoka na kuelekea kituo cha basi kuwahi basi la
kwenda kwao. Wakati huo huo wazazi kadhaa wenye magari wakawa wamekuja
kuwachukua watoto wao, mtoto akawaangalia wale wazazi nae akasema;
Mtoto: Dah wale ndio wazazi
mbona Mungu kaninyima
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE