Jamaa alikuwa anatafuta mbwa, akapita mtaa mmoja akakuta jamaa anauza mbwa kwa shilingi alfu 50 kila mmoja, lakini jamaa hakuwapenda,
JAMAA: Huna wengine? Hawa hawajanifurahisha
MUUZA MBWA: Ninae mmoja nyumbani namuuza alfu tano, ila huyo anajua kuongea
JAMAA: Duh twende ukanionyeshe....wakafika kwa jamaa, akaonyeshwa mbwa.
JAMAA: Umesema anajua kuongea?
MBWA:Ndio mi naongea, halafu ni poa ukininunua , nilishakuwa mbwa wa polisi nimekamata sana wezi mpaka nikapandishwa cheo kuwa mpelelezi mkuu wa kanda maalumu
JAMAA: Mi sitaki mbwa wa polisi
MBWA: Naweza kufanya kazi nyingine kama kukuletea viatu, au kwenda kununulia vocha za simu
JAMAA: Okay ntakuchukua. Sasa Mzee inakuwaje wale mbwa wa kawaida unawauza shilingi alfu hamsini na huyu mbwa anaongea unamuuza alfu tano?
MUUZA MBWA: Bwana tatizo la huyo mbwa muongo sana, hebu ondoka nae.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE