9 July 2012

Waraka wa kwanza kwa watembea wa miguu...


Sisi wenye vyombo vya usafiri baada ya kuvumilia kwa muda mrefu tumeona tutoe dukuduku letu kuhusu nyinyi watembea kwa miguu wa Tanzania hususani nyinyi wa Jiji la Dar aka Bongo. Watembea kwa miguu mnasababisha kero kwa siye wenye vyombo vya usafiri. Yapo mengi mnayofanya lakini hapa kwa waraka huu wa kwanza tumeamua kutaja machache.

i.               Kila mtu anajua taa zile zinazobadirika rangi kwenye njiapanda mbalimbali zinaitwa, 'taa za kuongozea magari’, hivi kwa nini na nyie eti mkiona taa ya kijani ina picha ya mtu mnaanza kuvuka barabara? Hamuoni mara ngapi mnakoswakoswa na vibajaji na bodaboda? Hamruhusiwi kuvuka mpaka sisi tuwe tumemaliza ishu zetu jamani, mnatuchanganya. Kazi ya zile taa zote pale barabarani ni kama ifuatavyo, taa nyekundu maana yake dereva punguza mwendo kama hakuna gari jingine endelea na ishu, pia hata ikiwaka kijani au njano kwa sisi madereva maana ya hizo taa haibadiliki, sasa nyinyi kwanini mnakuwa kimbelembele? Au kwa kuwa ni rangi ya chama basi mnajiona wajanjaa. Ok nategemea mmeelewa kuwa taa zile haziwahusu ni za kuongozea magari si kuongozea watu.

ii.        Service Road..jamani neno liko wazi kuwa hiyo ni barabara ya service ya magari yanayoharibika, binadamu service yao huwa hospitali kule walikogoma sasa mnatafuta nini service road jamani? Kutokana na msongamano hiyo barabara tumekubaliana wenzetu wenye usafiri wa bodaboda na bajaji na daladala waitumie kadri wanavyoona inafaa, nyinyi watembea kwa miguu tafuteni solusheni ya matatizo yenu. Hata mjengoni wanapoongelea miundo mbinu wanaongelea barabara za magari sio za watembea kwa miguu au huwa hamsikilizi? Kwanza swali la ziada mna muwakilishi mjengoni nyinyi? Wote walioko kule wanavyombo vya usafiri kama sisi, nani anawawakilishwa kwa kuwa mtwanga miguu mwenzenu? Tafadhalini hatuwataki kwenye service road labda kama hatuzitumii.

iii.           Inaitwa kwa kizungu Zebra Crossing kwa Kiswahili  alama za Pundamilia, kwanini nyie mmeamua kuwa ni sehemu za kuvukia binadamu, yaani lets be honest inaudhi sana. Mtu uko kwenye gari lako, umewasha AC, uko spidi 80, muziki mzito unapiga, mkononi una Blackberry unatuma TXT, ghafla mtu anaamua kuvuka barabara kwa kuwa kuna alama za pundamilia,  huu ukorofi utakuwa umepangwa na wapinzani kuharibu taratibu tu hakuna sababu nyingine. Jamani hebu niwaeleze, alama zile ziko kwa sababu kuu 2. Kwanza wataalamu wetu wameona kwenye sinema nyingi huko Ulaya, na wengine wamesoma huko, hizo alama zinachorwa sehemu nyingi barabarani kwa hiyo ili barabara zetu zifanane na za Ulaya ikaonekana ni vizuri na sisi tuwe na hizo alama. Pili barabara zikiwa nyeusi tu kwa muda mrefu siyo vizuri kwa hiyo unaweka alama hizo za mabaka meupe kuondoa monotony, kupamba barabara. Hata ulaya kwenyewe inajulikana alama hizo ni za Zebra Crossing yaana mahala pundamilia huwa wanavukia barabara sasa niseme nini zaidi?
Nashauri serikali itengeneze semina elekezi kule Ngurudoto ambapo watembea miguu wote waende wahudhurie semina kwa siku mbili ili kujua ukomo wao katika matumizi ya barabara.
Mkuu wa wenye vyombo vya usafiri 

No comments:

Post a Comment

SEMA USIKIKE