7 October 2012

SIKU YA HARUSI NITACHEZA AZONTO

Nilikuwa naongea na mtoto wa jirani kuhusu mipango na malengo ya maisha yake. Kwa kweli amenifurahisha sana maana anaelewa vizuri kila kitu kitakuwaje na amejipanga vizuri sana. Pamoja na mambo mengi ambayo ni wazi anajua atafanya nini, ni huu mpango wake wa kuoa. Pamoja na kuwa nimegundua kuwa hajaongea bado na wala hajakubaliana mke mtarajiwa, ni wazi hana wasiwasi kuwa khuo ndie atakae kuwa mwenza wake katika maisha. Kutokana na maelezo yake ni wazi ndoa kubwa itafanyika hapa mtaani mapema mwaka kesho. Kwa maelezo ya bwana harusi mtarajiwa wasanii wa bongo fleva na bongo muvi wote watakuwepo. Diamond atapafom na yeye mwenyewe bwana harusi atacheza azonto siku ya harusi. Kwa kweli nimefurahishwa sana na mazungumzo ya bwana harusi huyu hasa ukizingatia yuko nursery na ameshaamua akimaliza naursery tu anamuoa mtoto wa mwenye duka jirani ili wawe wanapata vitu bure.

No comments:

Post a Comment

SEMA USIKIKE