7 October 2012

USHAURI WA BURE KWA WALEVI WAPYA


Kuna msemo maarufu wa Kiswahili, Pombe si chai, na hili hudhihirika zaidi kwa wanywaji ambao ndio kwanza wanaanza kujifunza kunywa. Hapa najaribu kutoa ushauri ambao unaweza kuwapa majibu watakapojikuta katika hali mbalimbali baada ya kufakamia pombe, urabu, ngumu kumeza na kadhalika.
Tafadhali ieleweke kuwa kuwa matatizo haya hutokea kwa pombe zote zilizohalali na zisizo halali;
1.   Unaamka ghafla unakuta kimya kikuu na giza zito- mara nyingi ni dalili za wazi kuwa umelala baa na wamekufungia, ni busara kutokupanik na kuendelea kulala mpaka watakapofungua kesho yake, kama umeoa au umeolewa ndoa yako iko pabaya.
2.   Unakuta kila mtu anakuangalia ana cheka – Je uko juu ya meza unacheza? Umejikojolea? Au miguu imekataa kufanya kazi. Au umevua nguo zote unajiita John Cenna? Ni bora uwataarifu wote kuwa wewe una pesa ndio maana umelewa mno, japo hilo litaalika vibaka wakuandame.
3.   Unajikuta ghafla unatoka damu mdomoni na puani- ni dalili kuwa imepigwa, kikubwa ni nyamaza usianze kujitetea au kuonyesha kuwa umeonewa, utapigwa zaidi, we omba msamaha tu.
4.   Uko kwenye bar hukumbuki uliingia  saa ngapi na pia hakuna mtu unaemtambua, wala hata mtaa ulipohuelewi- Hii ni mbaya mtu wa Masaki unaweza ukawa uko Manzese, au unadhani uko kwa Rick Ross Kinondoni, kumbe uko Dar Live Mbagala, kuolewa ni rahisi sana katika mazingira haya
5.   Unajikuta unalilia penzi la mhudumu- Hizi ni dalili mbaya ambazo zinaweza kukusababisha uje kupigwa tena, maana mara nyingi unajiona kuwa hakuna mwanamke mzuri kama huyo na uko tayari kuruka kung fu kwa ajili yake,

No comments:

Post a Comment

SEMA USIKIKE