4 October 2012

UNA DAMU YA KABILA GANI?

1. Ukiona kila unapotaka kusema FANTA, unasema FANDA ujue una damu ya Kihehe
2. Ukiona kila unapotaka kusema SODA, unasema THODA ujue una damu ya Kipare
3. Ukiona kila unapotaka kusema KAFARIKI, unasema KAFWALIKI ujue una damu ya Kihaya
4. Ukiona kila unapotaka kusema CEILING BOARD, unasema SINGLIBODI ujue una damu ya Kichaga
5. Ukiona kila unapotaka kusema MTOTO, unasema NTOTO ujue una damu ya Kimakonde
6. Ukiona kila unapotaka kusema UJI, unasema UCHI ujue una damu ya Kikurya
7. Ukiona kila unapotaka kusema ANAKUJUA, unasema ANAKOJOA ujue una damu ya Kijaluo
8. Ukiona kila unapotaka kusema NYUMBA YETU, unasema NYUMBIYITU ujue una damu ya Kingoni
9. Ukiona kila unapotaka kusema CHAI YA MOTO, unasema KYAI KYA MOTO ujue una damu ya Kinyakyusa
10. Ukiona kila unapotaka kusema TV, unasema TIWI ujue una damu ya Kihindi

1 comment:

  1. Kwa kuongezea. Ukitaka kusema "mkate" au "mkeka" badala yake ukasema "nkate" au "nkeka" basi una damu ya kipemba

    ReplyDelete

SEMA USIKIKE