Mdada
alienda super-market kununua kuku, bahati mbaya kwenye friza kulikuwa na kuku
mmoja tu, muuzaji akamtoa akamuweka kwenye mzani, akaonekana ana kilo moja na
robo. Mdada akamuuliza muuzaji,’Huna mkubwa zaidi?’ Muuzaji akamchukua yule
kuku na kujifanya kamrudisha kwenye friji, halafu akamtoa tena kwenye friji na
kumrudisha kwenye mzani, safari hii akagandamiza mzani kwa gumba, kuku akaonekana
ana kilo mbili. Mdada akasema ‘Duh afadhali huyu mkubwa kidogo, naomba unifungie
nawachukua wote wawili’

No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE