KATIKA
kipindi kirefu sasa nimekuwa naangalia uwezekanao wa kuoa. Hii ishu ya kula
ugali mbichi niliousonga mwenyewe kiukweli inaniudhi. Nikiwacheki jamaa zangu
tuliocheza pamoja utotoni wote wana wake zao na watoto kadhaa, tena wengine
wana zaidi ya mke mmoja na tukikutana mtaani utakuta wanaelekea kwenye
michepuko yao, kimsingi wako bizi sana. Mimi nimekuwa napanga na ma mimi niwe
na mke. Jambo moja ambalo nimeamua ni kuwa sioi Bongo hata iweje, toka hizi
instagram na whatsap zimeingia mjini, wadada wa hapa wamekuwa na timu zao, hebu
fikiria ukioa mke mwenye timu ya nguvu si ndio utatukanwa instagram kila
asubuhi. Lazima nioe kitu toka nje ya nchi, hii kwanza itasaidia hata kuleta
mabadiliko katika ukoo wangu, na Taifa letu kwa ujumla. Pili italeta sifa, japokuwa mtu mmoja kwenye ukoo
wetu kaoa mgeni toka nje ya nchi, tatu itapunguza umbeya, maana ntaleta mke
hajui Kiswahili, hivyo wifi zake wakianza mafumbo, ye haelewi anacheka tu.
Halafu na yeye mwenyewe atakuwa hana cha kuongea hata akienda saluni, mambo
yetu yatabaki kuwa siri. Nimeshaanza utafiti, nimekuwa natumia muvi mbalimbali
kujifunza Taifa gani linafaa kuoa. Kwanza nimeshajua kuwa siji kuoa Mnaijeria,
we angalia muvi zao, wadada wa Kinaijeria wagomvi hao, hawaoni tabu kulianzisha
saa yoyote, halafu hawaoni tabu kukuendea kwa mganga. Wanaijeria siwataki
kabisaaa. Baada ya kuona muvi za akina Kim Kadeshian na vituko vya baba yao,
sitaki kuoa Mmarekani kabisa, hebu fikiria baba mkwe kabadilisha jinsia kawa
mdada, sasa unamwita baba mkwe au unamwita mama mkwe? Wamrekani tupa kule. Ila
mpaka sasa roho yangu imewaangukia Wahindi, nimepanga kumuoa Mdosi. Yaani sauti
za mabinti wa Kihindi wakiimba utapenda, sura zao wote nzuriiii, halafu sio
wagomvi wapole yaani kwa kweli hapo ndio chaguo langu. Ila kuna changamoto kubwa
sana kumpata mdada wa Kidosi hapa kwetu. Kwenye muvi hawa wadada utakuwakuta
kwenye bustani kama ya Mnazi Mmoja wanaimba na kufukuzana na wapenzi wao, sasa
mbona hapa kwetu sijawahi kuwaona wapenzi wa namna hiyo wakifukuzana na
kuparamia miti wakiimba kwa mapenzi. Mimi nimeshajifua naweza kuimba na kucheza
wimbo wote wa Kuch kuch kotaye. Mkimuona binti wa Kihindi wa umri wa kuolewa
nielekezeni ili nikamuimbie niweze kupata mke. Hapa Kazi moja tu, kuoa Mhindi
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE