Kuwa
mzee kuna shida zake nakwambia. Kuna wakati unakaa unawaza halafu unacheka peke
yako. Vijan wa siku hizi wanajifanya wajuaji lakini ukiona wanayofanya
unachekea tumboni maana wakijua unawacheka wanaweza kuanzisha timbwili la dada
yao Asha Ngedere. Leo asubuhi nilikuwa nawaza hii ishu ya ndoa siku hizi,
nikaanza kucheka peke yangu, mjukuu wangu kaniuliza nacheka nini nikamwambia
nimekumbuka sinema za Chale chapmlin. Kwanza enzi zetu si mwanaume wala si
mwanamke wazazi wako waliweza kukuchagulia mwenza wako. Unaweza kuwa umekaa
nyumbani baba yako anakuja anakwambia, “Mwanangu nimemuona binti ya rafiki
yangu mmoja nimeona anakufaa, nimekwisha ongea na rafiki yangu na amaekubali
muoane” Mchezo unaisha hapo mzee atafanya shughuli zote za kulipa mahari na
kadhalika wewe kazi yako ni kuvuta mke ndani. Siku hizi sasa, ubishi umezidi
basi wazee tumewaachia kazi hiyo wahusika ndio hapo kila siku kijana akitoka
klab anakuja na mchumba mpya. Siku
akiaamua kuwa kapata anaemfaa basi linaanza sekeseke la kuwambia mumchangie eti
kwa ajili ya sherehe, sasa kuoa umeoa wewe kwa kupenda mwenyewe, huu mzigo wa
kugharamia harusi yako kwanini uwachangishe watu? Enzi zetu hutukuchanga lakini
watu walialikwa kwenda kula na utakula vizuri chakula kilichotengenezwa na bibi
harusi mtarajiwa, siku hizi unachanga halafu hata chakula hupati, ukipata
chakula chenyewe utadhani ni kwa ajili ya wanafunzi wa boding, kibaya kweli.
Mke unafika nae nyumbani kumbe hajui kupika, mnaishia kula chips zege cha baa
kila siku, jamani kwanini nisicheke? ni halali nitoe machozi
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE