MWAKA
2020 mjue kabisa kuwa nakuja kugombea
Urais. Tena niko tayari kufanya
kazi hiyo bila mshahara, wala gari, ntakuwa napanda Bajaj, kwenda ofisini, na
kwa taarifa ntaendelea kuishi ghetto langu hilihili, ili niwe karibu zaidi na
wananchi wangu. Mimi sio mwanasiasa kwa hiyo maneno mengi sina nia na madhumuni
ya kugombea urais ni kuhakikisha Whatsapp naipiga marufuku. Nataka niwataarifu
mapema hakuna kitu kinaniudhi kama
whatsapp, yaani hii kitu ndilo jipu la kwanza nitakaloanza kulitumbua mara tuu
baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kunitangaza Rais. Unajua hii kitu imefikia
imewazuzua watu kiasi cha kwamba kuna watu wakiamka kitu cha kwanza ni kufungua
whatsapp kucheki meseji, na wakishaanza siku basi ujue hapo kila dakika tano
wanaangalia simu kama kuna mesej mpya. Mtu mmoja anakuwa kwenye magrupu kumi,
na kila moja linatuma mesej hamsini kila saa na mtu anataka kuzisoma zote,
yaani anafanya kazi saa ngapi? Hata kulala wengine hawalali vizuri kwa
kutegeshea kusoma meseji, au kutuma meseji. Whatsapp ni jipu. Watu wanaogopa
kuzima simu hata wakiingia kwenye ibada wanaogopa isije ikatokea mesej
zikaingia wakati wamezima simu. Kesho
au keshokutwa naenda andikisha chama Chama cha Wapinga Whatsapp
Tanzania-CHAWA. Ndugu zangu jiungeni
kwenye chama changu cha CHAWA tuliondoe jipu hili. We fikiria unamchangua mtu
awawakilishe sehemu badala yake anatumia muda huo kuchati halafu anadai yuko
kwa ajili yenu, utapeli mkubwa, wabunge wa chama changu hawatakuwa wanatumia
whatsapp kamwe ili wahakikishe wanalinda maslahi ya wananchi. Unajua siku hizi
unaweza ukawa umekaa na mpenzi wako kumbe anawasiliana na mpenzi mwingine na
wewe uko hapohapo na picha utapigwa itatumwa ikiwa na maelezo, niko na fala, unajua hilo? Halafu kinachoniudhi kuliko yote ni hawa
madreva wanaoendesha huku
wanachat, yaani hawa ndio ukisikia chizi fresh au kubwa jinga basi ndio hawa.
Yaani jitu limesoma vizuri, lina pesa nzuri linaaminika kazini, lina gari zuri,
lina familia inalitegemea halafu linachezea maisha yake na ya wengine kwa
kuchati wakati linaendesha gari, yaani bila wasiwasi tulisaidie lisije likafa au
likapata ulemavu na kutesa wanafamilia tupige marufuku chanzo nacho ni
whatsapp. Wananchi wote tujiunge na CHAWA.

No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE