JAMAA mmoja alikuwa na tatizo la kukojoa kitandani. Ikafikia anataka kuoa lakini aibu ikawa inamzuia hata kutafuta mchumba, akaamua kwenda kwa mganga kupata matibabu.
MGANGA:Tatizo limeanza lini?
JAMAA: Kiukweli toka nilipokuwa mdogo. Nimepigwa sana na wazazi wangu lakini wapi. Kila nikilala huwa ninaota mtu anakuja ananambia 'Aise twende tukakojoe' Nikiamka nimesha kojoa
Mganga akamchanja jamaa chale nyingi mwili mzima na kufanya vimbwanga vingi sana kisha akatoa masharti
MGANGA: Sasa nimeshakutibu hivyo ukiota tena hiyo ndoto, akija akikwambia tukakojoe, we mjibu kwa ukali mwambie nimeshakojoa, sawa?
Jamaa akaondoka akiwa na uhakika kesha pona. Kesho yake akarudi kwa mganga, tena akarudi huku analia
MGANGA: Vipi tena mbona unalia?
JAMAA: Mzee tatizo limekuwa kubwa
MGANGA: Kivipi?
JAMAA: Jana nililala vizuri na yule jamaa akaja. Kama kawaida akanambia 'Twende tukakojoe" Na mimi nikakumbuka masharti yako nikamkemea kwa nguvu na kumwambia ' Toka shetani mkubwa, mimi nimeshakojoa' Si ndipo akanambia, 'Basi poa twende tukanye' Mzee chumba changu hakifai
Teh teh teh
ReplyDelete