24 October 2016

USITUME MESEJI HUMU MUME WANGU ANAWEZA KUUSOMA

WANAUME kadhaa walikuwa kwenye semina kanisani wakipewa mafunzo ya namna ya kuishi vizuri katika ndoa. Mchungaji akawauliza ni wangapi wanakumbuka mara ya mwisho walipowaambia wake zao kuwa wanawapenda. Wengine wakasema ni siku hiyohiyo wengine mwezi, wengine hawakumbuki mara ya mwisho kutamka kitu hicho. Mchungaji akawaambia kila mtu amtumie mke wake ujumbe rahisi tu. NAKUPENDA MKE WANGU. Baada ya hapo waliambiwa wabadilishane simu na kila mtu asome majibu ya simu yaliyorudishwa. Hapa chini ni baadhi ya majibu yaliyopokelewa;
1. Mume wangu umeshamtia mimba msichana mwingine?
2. Labda miaka hiyo, sio leo
3. Sina hela, ulizochukua zinatosha
4. Umefanya nini tena? Nimechoka kukuwekea dhamana
5. Sijakuelewa
6. Wimbo mpya huo?
7. Siamini lazima naota
8. Usiponambia ujumbe huu ulikuwa unaupeleka wapi, usirudi leo!
9. Mume wangu, mara ngapi nakwambia uache pombe?
10. Nani mwenzangu?

11. Samahani usitume ujumbe kama huu kwenye simu hii, mume wangu anaweza kuusoma, ntakupa namba yangu ya siri

No comments:

Post a Comment

SEMA USIKIKE