Ndugu
zangu leo nimekasirika. Kuna watu wameniudhi nimeshindwa hata kunywa chai
asubuhi. Kiukweli sasa hii imevuka mipaka nasema hii siikubali kabisa. Mambo
kama haya ndio yanaweza kumfanya mtu akaamua kurudi kijijini kwao kuomba msaada
wa mizimu ya kwao kulipa kisasi au kama ni mtoto wa mjini kuchukua uamuzi wa
mwendokasi na kuruka vichwa sehemu za heshima. Yaan najiuliza bado nini hiki?
Nauliza tena nini hiki sasa? Hivi kweli mnaona mnafanya jambo la kawaida
kabisa? Nasema kiukweli baada ya muda mfupi nitamtoa mtu kongosho, mi sio mtu
wa mchezomchezo, ulizeni jamani, ulizeni mtaani kwetu watawaambia kuwa huwa
sipendi utani. Kwanza kabila letu hatupendi maneno sisi ni kazi tu, sasa
nauliza nani amebadilisha sauti ya mwito wa simu yangu? Nikipigiwa simu mdada
mmoja anawahi kimbelembele anaanza kujibu eti, ‘Asante kwa kumpigia malkia,
malkia ni mke wa mfalme. Malkia atapokea simu yako sasa hivi’ Aise mie malkia? Nauliza
na ndevu na mustachi huu mnaniita mie malkia? Nawaona wengine mnacheka mnacheka
nini? Kuna la kucheka hapo wakati mwanaume mzima naitwa malkia? Huu utani sasa
umevuka mipaka namsaka huyu aliyewaambia naitwa Malkia na pia mtaniambia
kwanini hamkuniuliza mpaka mkaamini kuwa naitwa Malkia na kuruhusu kila
anaenipigia anatangaziwa kuwa mie ni Malkia. Dah najisikia kulia kwa hasira. Nimeanza kuchekwa mtaani, yaani karibu
kila mtu mpaka vitoto vikiniona vinacheka, ndugu zangu wananiuliza lini
nimebadili jina, wengine nawaona wananiangalia kiajabu ajabu wanashangaa
kwanini najiita jina la malkia. Sasa sikilizeni naenda kulala nikiamka nikute
mmefuta hako katangazo kenu kanakoniita mie majina ya ajabu. Sitaki kurudia
tena, mi mbayaa ohh shauri zenu. Nasema tena nikiamua kurudi kwetu kuongea na
babu nimtaarifu kuwa mjukuu wake anaitwa malkia, kitakachowatokea mi simo. Haya
kwa usalama futeni hako kasauti. Sipendagi ugomvi.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE