Yaani
jamaa wameniudhi kabisa wameniondoa kwenye mudi wakati nilikuwa katika furaha
kubwa. Kwa mara ya kwanza nilikuwa nimesuka dili likatiki. Unajua siku hizi
milango yote imefungwa madili hayakubali kabisa, watu tuko hali mbaya kila kona
mtu unadaiwa, anaekudai nae anadaiwa, yaani sijui nani anazo. Ukienda kukopa
unaambiwa unaetaka kumkopa kenda kukopa ili amlipe anaemdai. Hali ngumu, sasa
mimi nikawa nimecheza mchezo fulani, ukakubali, mfukoni nikawa na kitu kama
laki hivi, laki ni pesa siku hizi. Kwa kuwa ilikuwa majira ya saa sita mchana, nikaona
niingie kwenye baa moja maarufu ambayo mchana inakuwa restoranti, nile chakula
safi kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu. Nikatafuta kiti kwenye kona,
gazeti langu la Risasi Jumatano nililo linunua njiani nikalikunjua na kuanza
kusoma. Ilipita kama dakika kumi, sioni muhudumu, nikaangalia huku na kule na
kumuona jamaa mmoa amaevaa tai nikajua yule ndie meneja, si unajua mameneja wa
baa siku hizi lazima wavae tai, hata kama joto liko kiasi gani, basi ile
kumuuangalia tu, hapo hapo akajua tatizo liko wapi akamtuma binti mmoja aje
kunisikiliza. Binti alipokuja akaniuliza nikaagiza chakula na kinywaji na
kuanza kusubiri, nikaendelea kusoma gazeti langu, ghafla akaja mdada mwingine
na mopu la kupigia deki, akaniomba ninyanyue miguu apige deki. Sikuwa na makuu
nikanyanyua miguu wakati nimenyanyua miguu, akaja mdada mwingine na bakuli la maji
na kitambaa akanambia ninyanyue mikono anataka kufuta meza, hee nikanyanyua
gazeti langu juu. Hapo ndipo nilipojua kuwa na mimi naweza sarakasi, nilikuwa
nimekaa kwenye kiti, huku nimenyanyua miguu na mikono. Wadada hawa ambao
walionekana wamegombana maana walionyesha wazi kila moja hana mpango wa kuongea
na mwenzie lakini waliweza kunipa amri hizi kali. Huwezi amaini ilionekana eti
wameamua kufanya usafi kwenye meza yangu tu, mmoja anapiga deki chini mwingine
anasafisha meza. Hatimae wakaniruhusu nishushe viungo vyangu, wakaondoka. Muda
ukawa unayoyoma simuoni wakuleta chakula wala kinywaji. Nikaanza kujiuliza mimi
nina mkosi gani mbona jamaa waliokuja baada yangu walikuwa tayari wamepewa
chakula? Hela ninayo, na nilikuwa nimejipanga kula vizuri hawa jamaa hapa
wameamua hawanipi chakula wala kinywaji. Nikaamua kulianzisha…..si unajua
kabila letu huwaga hawajui kuongea, tukisema neno ‘swela’ hapo ujue ni kipigo tu.
Nilipomaliza kazi nikaondoka na tai ya meneja. Sipendagi ujinga mimi.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE