11 October 2016
TUWE NA HURUMA JAMANI, INGAWAJE INAUMA
Kuwa na huruma sana inaponza sana, kwa mfano wa karibu ni mimi. Unajua
mimi ni mtu mwenye huruma sana, na hii inanikosti. Lakini bahati mbaya
hiyo ndio tabia yangu, siwezi kubadilika. Unajua kwa mfano isingekuwa
huruma yangu ya hali ya juu leo hii ningekuwa sinywi pombe kabisaaaa
unaonaee. Lakini mara nyingi nikiwa na glasi ya mwisho ambayo huwa
najisemea baada ya glasi hii sinywi tena, utaona huruma yangu inaanza
kunisuta. Maana naanza kufikiria ni watu wangapi ambao maisha yao
yanategemea wanywaji kama mimi kuendelea kunywa? Kuna wakulima wa ngano
ambao ikiwa wanywaji wote tutaacha kunywa na wao watakosa kipato cha
kuuza mazao yao kwa watengeneza pombe, maisha ya watoto wao itakuwaje?
Haya baada ya hapo kuna hizi kampuni za kutengeneza pombe, tena siku
hizi ukienda kwenye makampuni makubwa kuna wakurugenzi, wakurugenzi
wasaidizi, kaimu wakurugenzi, mameneja, wahasibu , wahudumu wa ofisi,
madreva, wafanyakazi viwandani, watu wa masoko, wenye baa, wahudumu wa
baa, yaani nikiwaza kuacha pombe naanza kufikiria watoto wa hawa watu
wote wananitegemea mimi, halafu kitendo cha kufanya ukatili mkubwa wa
kuwanyima haki yao ya kuishi kwa ajili ya ubinafsi wangu tu kinanisuta
sana? Tena siku hizi unakuta mpaka wasanii toka nje wanatakiwa kuja
kuponea fedha zangu ili watoto wao waende shule, kwa kweli huruma yangu
naona ni muhimu kuliko ubinafsi wangu. na hapo ndipo huwa naagiza nne
mfululizo, sio kwa sababu napenda pombe jamani ni huruma kwa hawa wote
ambao maisha yao hapa mjini yananitegemea umeonaee. Tujitahidi jamani
ili kusaidia wenzetu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE