Mdada
mmoja jirani yangu , alikuwa kila siku ananilalamikia kuwa kuna rafiki yake hataki
kulipa deni la nguo na viatu alivyochukua siku nyingi, jambo ambalo limeua
mtaji wa biashara yake, mbali zaidi amekuwa hata simu zake hapokei. Kwa siku
anampigia hata mara kumi lakini hapokei na kila akienda kwake hamkuti. Kwa
kweli nilikuwa namuonea huruma na pia nilikuwa naumia mimi maana yake alikuwa
anakuja geto kila asubuhi mara aombe sukari, mara chumvi mara nauli, vocha ndio
usiseme. Leo asubuhi kanigongea, nikaamka nikijua napigwa mzinga mwingine
asubuhisubuhi, badala ya masikitiko akanipa bahasha ndani nikakuta alfu hamsini,
wakati nashangaa akasema ‘Zako
hizo na pole kwa kukusumbua kwa muda mrefu’. Nikamuuliza za nini? Akanijibu
aliyekuwa anamdai kamlipa, hivyo ameona ni haki nipate japo kidogo.
Nikashukuru, na ndio nikamuuliza kwani kimetokea nini mpaka akalipwa? Hapo
ndipo aliponipa stori nzima. Baada ya kuona simu hazipokelewi basi akamtumia mdeni
wake ujumbe wa maneno ufuatao. ‘ Shosti
sikupigii kwa ajili na kukudai nilikuwa nakwambia tu kuwa kuna mabinti
wawili walikuwa wanamgombea mumeo, wametandikana sana, mumeo alikuwa pembeni
anaangalia tu. Mmoja akapigwa akakimbia basi mumeo akaondoka na yule mshindi
kamkumbatia kiunoni’. Haikuchukua hata dakika tano mdeni wake akampigia,
hakupokea. Katika nusu saa zilipigwa missed call kama 30. Baadae mdeni akaanza kutuma meseji,
‘Ugomvi ulikuwa wapi?’ ‘Walielekea wapi na mume wangu?’, ‘Mwanamke mwenyewe
unamjua?” , ‘Shosti tafadhali nambie kumbuka urafiki wetu shosti’. Baada ya
hapo zikaanza missed call tena, ambazo hazikupokelewa. Ndipo ikaja mesej tamu,’Hela zako ninazo tukutane wapi
nikupe unielezee mkasa mzima?’ Hapo ndipo jirani akajibu. ‘Shosti nitumie
kusudi nipatie na usafiri nije nikupeleke walipoenda, kiukweli alichofanya
shemeji ni cha aibu, twende tukamkomeshe’. Hazikupita sekunde chache deni
likalipwa na hela za usafiri juu. Hapo ndipo jirani yangu akaenda kwa wakala
akatoa fedha zake kisha akazima simu na kuendelea na shughuli zake kwa raha
zake. Jirani yangu si mtu wa mchezo mchezo
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE