Chungu ndio hicho kiko jikoni mambo yamekaribia kuiva, Trump ndo keshakuwa Rais wa marekani. Nimeona nitoe wosia kwa ndugu zangu Wabongo-Wamarekani, nadhani kipindi hiki wanahitaji ushauri nasaha. Kwanza hongereni kwa uchaguzi safi wa kidemokrezia, Kibongobongo lazima kupeana hongera kwa kila kitu hata ukimaliza msiba utaambiwa ‘Hongera kwa kumaliza msiba salama’. Hili muanze kulizoea maana najua muda si mrefu mtalazimika kurudi nyumbani. Nyumbani ni nyumbani. Kutokana na maelezo ya Rais wenu shughuli ya kurudi itaanza karibuni nimeona nichukue nafasi hii kuwatayarisha na hali ya huku. Kwanza huku umeme sehemu nyingine unazingua, tafadhali njoo na power bank, usitegemee kununua za huku, utakasirika maana powerbank za huku majanga matupu unaweza kununua ikafanya kazi au ikafa baada ya siku mbili, au ukauziwa ‘kanyaboya’ kabisaa. Neno kanyaboya maana yake utauziwa ndichosicho. Kifupi njoo na pawabenki yako. Pia nashauri chaji kabisa simu huko halafu uje huku maana inawezekana ukalazimika kufikia kijijini kwenu ambako umeme hauko kabisaa, wanakijiji wanategemea kuchaji kijiji jirani kwenye duka lenye jenereta. Weka pesa pembeni ya kununua ‘airtime’ huku hakuna WIFI za bure, ukifika kuna kampuni kibao za line za simu zinatoa huduma ya intanet lakini kuna nyingine bomu kishenzi, watakuambia lipa elfu utapata internet siku nzima kumbe wao siku yao ni masaa matatu tu. Uliza kwanza wenyeji wakuambie. Usafiri wa haraka na gharama ndogo huku ni bodaboda, kutokana na ubahili mliojifunza huko, huo ndio usafiri mtakao ona unawafaa lakini tegemeeni kuvunjika miguu sana mapema kama mtang’ang’ania usafiri huo. Kwa watoto ambao mtalazimika kurudi huku na wazazi wenu, eleweni kuwa huku mzazi wako akikupiga hakuna kesi, labda akuuwe, hivyo mkija huku hakikisheni mna adabu, ukimjibu hovyo mzazi wako ruksa jirani kuingilia kesi na kukupa mkong’oto na umma utamuunga mkono. Hakuna kazi huku, hata kama una digrii na kiingereza cha kimarekani haisadii men, tena afadhali zamani babako kama anamjua mtu anaemjua mwanasiasa mjumbe wa bodi fulani ungepata kazi, siku hizi huku yuko mtu anaitwa JPM mchezo huo hakuna. Kwa mayanki mnaojifanya mahendsam, Mademu wa hapa huwa hawachangii kulipa ukimtoa out, hapo ujue bili zote zako hata kama ana hela kuliko wewe, hivyo ukija kichwakichwa aukijua demu atajitegemea wakati wewe ndio umemwambia muende mkale chakula cha jioni au muende klabu, utalia, tena wana kamtindo kakusema 'anakuja na mwenzie kusudi awe na kamapani'. Wadada mkija huku sio unavaa kila nguo kila mahala, ukienda sokoni na kimini usishangae wakati ukaanza kushangiliwa kama supasta,utafanyiwa mambo mazito hadharani, ukienda polisi kushtaki kuwa unanyanyaswa utafunguliwa mashtaka kwa kutembea utupu shauri yako usiseme sikukuambia. Ishu za kukumbatiana hadharani kuonyesha mnapendana acheni hukohuko, mtapigwa mawe huku.
Na kama ulikuwa huwasiliani na nduguzo ishu yako itakuwa ngumu kidogo, maana watu wataabaki wanakuangalia tu unapoharibikiwa wakucheke.
Karibuni
sana
Huku 95% tunatumia kuni basi jiko la gec mwachie trump
ReplyDelete