Na Dotto Mwaibale
WANANDOA
wanaojimwa ujumba na wenza wao wametakiwa kwenda kushitaki dawati la
jinsia yaliyopo vituo mbalimbali vya polisi ili kupatiwa utatuzi wa
changamoto hiyo.
Mwito
huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva wakati
akizindua maonyesho ya dawati la jinsia na watoto katika viwanja vya
Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo ambayo yalishirikisha wadau
mbalimbali kutoka Hospitali ya Amana wilayani Ilala na wananchi.
"Ukatili
wa kijinsia si kupigana na kutukana hata mume na mke wakinyimana
unyumba pia ni ukatili wa kijinsia hivyo anayejimwa hasione aibu aende
kushitaki dawati la jinsia katika kituo chochote cha polisi" alisema
Lyaniva.
Lyaniva
aliwataka wananchi wanao fanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenda
kwenye dawati hilo kupata ushauri kutoka kwa maofisa wa polisi
waliopatiwa mafunzo ya kutatua changamoto hiyo.
Katika
hatua nyingine Lyaniva aliwaagiza maofisa wa polisi wa dawati hilo
kutotoa nje siri za watu wanaopeleka malalamiko yao katika dawati hilo
kwa kufanya hivyo ni kukiuka utaratibu wa kazi.
Aliwaasa
wanandoa kuwa na mshikamano na upendo ili kuwa na familia bora na yenye
maadili jambo litakalosaidia kutokuwepo kwa watoto waliokosa maadili na
kujiingiza kwenye makundi ya kiovu kama panya road.
Lyaniva
aliwaomba wanawake pale wanapopata mafanikio ya maisha kupata fedha au
kupanda vyeo kuacha kuwadharau waume zao ili kuepusha kuvinjika kwa ndoa
zao.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Temeke Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,
(SACP), Gilles Muroto amewataka wananchi wasiogope kwenda kutoa taarifa
za ukatili wa kijinsia katika vituo vya polisi kwani malalamiko yao
yatasikilizwa kwa faragha na maofisa maalumu wa jeshi hilo.
Maonyesho hayo yamedhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN).
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva (katikati), ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia wakati akizindua maonyesho ya dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Temeke viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Chang'ombe (OCD) Msuya, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Lucy Tesha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Gilles Muroto na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Vedastus Chambu kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini. |
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Lucy Tesha akihutubia kwenye uzinduzi huo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wadau na wananchi wakifuatilia hutuba za mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva.
Maofisa Wanawake wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia wakiwa kwenye Maonyesho hayo.
Wananchi na wadau wengine wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi
Wananchi na wadau wengine wakiwa kwenye maonyesho hayo.
Mrakibu wa Jeshi la Polisi, (SP), Faidha Suleiman (kushoto), ambaye anashughulikia dawati la jinsia Makao Makuu ya jeshi hilo akimkabidhi Mgeni rasmi DC wa Temeke machapisho mbalimbali ya ukatili wa kijinsia ikiwemo miongozo ya uanzishaji wa dawati la jinsia na watoto ndani ya jeshi hilo.
Mrakibu wa Jeshi la Polisi, (SP), Faidha Suleiman (kushoto), akimuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Temeke kuhusu kazi kubwa inayofanywa na jeshi hilo kwenye idara ya dawati la jinsia.
Wananchi wakipata machapisho mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE