Oya
washkaji naona sasa niongee lugha mtakayonielewa, mwaka huu lazima tubadilike
au vipi? Kuna watu wanaboa mpaka basi
sasa nimeona niwaibukie humu mnielewe. Nianze na washkaji wa Ubungo kituo
cha mabasi yaendayo mikoani, aise hivi nani aliwaambia mradi mtu anapita karibu
na hicho kituo basi lazima anataelekea Moshi Arusha Mwanza Iringa au Njombe? Yaani kila siku napita hapo
naelekea home Ubungo hamchoki kunisumbua eti niende kwenye miji hiyo nasema
nimechoka mnaboa, anaesafiri si ataingia ndani kuafuta tiketi? Kwanza kuingia kiyuoni nako ni shida tupu,
mmeweka milango ya chuma ya kuzunguka, mtu ukija na tenga lako kubwa hamruhusu
apite geti kubwa eti lazima apite kwenye kamalango hako kakuzunguka ambako
hakatoshi kupitisha tenga, mnataka afanye miujiza, au yote hii kusudi watu wakodi
vitorori vyenu ambavyo mnaviruhusu
kupita kwenye geti kubwa mnaboa sana mjue. Mtu achukue mzigo wangu halafu apite
geti ambalo mi siruhusiwi kupita tukipotezana si ndio mzigo wangu umekwenda na
maji? Mnajua mnaboa aise. Halafu
mtindo wa kuuza tiketi yuzd pale mlangoni wakati wa kuingia acheni mwaka huu,
ntakuja lianzisha pale tutaishia kugawana majengo ya serikali mmoja magereza
mwingine hospitali ohoo. Halafu kamtindo kanyie makonda kuruhusu watu kuja
kuhubiri bidhaa zao kwenye mabasi acheni mwaka huu, mtu umeamka kwenye saa tisa
usiku uwahi basi la saa kumi na mbili asubuhi ile unajinyoosha kupunguza
usingizi unasikia, “Samahani ndugu abilia Je, unachunusi au unanuka kikwapa?
Je, soksi zinanuka? Usikonde tunakuletea dawa ya kunywa ya Anko K inasaidia
sana, hata mimi nilikuwa nanuka kikwapa siku hizi sinuki kabisa kwa ajili ya
bidhaa hizi” Aise mnaboa sana mjue.
Halafu
hivi nyie machinga wa Kibaha mabasi yamewakosea nini? Basi likiingia kituoni
Kibaha lazima kila machinga aligonge kwa ngumi, yaani sijui ndio masharti ya
waganga wenu kuwa mkitaka kuuza basi basi likiingia kituoni pigeni ngumi, yaani
kama ndio umetoka Dar na umeshaanza kupata kausingizi, unaweza kukurupuka
ukadhani labda basi linapata ajali.
Mjue
mnaboa sana kwa kweli
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE