Yaani
mi naona nina kamakosi fulani, toka nizaliwe sijawahi kupata mrembo wa nguvu.
Yaani kila mara inatokea ishu ya kuniwekea kipingamizi cha kupata mrembo ambae
ana mvuto wa pekee. Yaani naona wazi kuna mkono wa mtu. Kuna watu sijui roho
zao zikoje, wao wanapenda kuona mtu anateseka hata kama wao hawapati kitu,
yaani ni roho mbaya tu imamfanya
mtu ana kuwekea kagundu fulani basi warembo unapishana nao, wanakupita hivi hivi
mubashara hawakuoni kabisa hata uwe umevaa nini. Kwa upande wangu na hili gundu
limeanza miaka mingi sana kwanza nilikuwa sijalistukia, lakini sasa nimesha jua
mambo sio sawa, kuna haja ya kutafuta mtaalamu, nisafishe nyota. Nyenzo moja
muhimu sana ukitaka kupata warembo wa ukweli ni kuwa na simu inayoenda na
wakati. Nimegundua kuna mtu kachafua nyota yangu ya kupata simu kali. Unaweza
kucheka lakini hilo ndilo gundu nililo logelezwa, nyota ya kupata simu za
kisasa imefukiwa kaburini. Warembo wa ukweli wanamaindi sana aina ya simu
uliyonayo, sasa mimi nimefanyiwa kitu kila mara nakuwa sina simu inayoenda na
wakati. Enzi zile wakati simu za twanga pepeta zinatamba, mi nilikuwa sina simu
kabisa, warembo wote wa ukweli walinikataa sababu hiyo. Nikahangaika nikaja
kupata kasimu kangu ka twanga pepeta, kumbe warembo wamehama wanataka watu
wenye blek beri, kila ninae jaribu kumuingia akishagundua nina twanga pepeta
ananitolea nje tena kwa kashfa. Nikajinyima nikaja kupata blek beri yangu, nikawa
nairingishia hata kujaribu kuwaonyesha, warembo kila nilipowakuta, baada ya
muda nikagundua wananicheka kumbe wajanja
walishahamia simu nyingine, watu wakawa wanakutana whatsapp sijui insta, mie
nikawa siko huko, basi nikachakalika nikapata na mie simu yenye whatsapp, ile
naanza kujisifu nakuta wameanza kutumia simu za kupangusa, nimestrago nimepata
ya kupangusa hawaniangalii mpaka nipate iphone, jamani nina mkosi gani? Sasa
kununua iphone ni mtihani, nikijinyima sana naweza nikawa na iphone mwisho wa mwaka , lakini najua tu
staili nyingine ya simu itakuwa imeanza , siku nikimjua aliyeniroga namtoa
kongosho
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE