Je,
umerogwa? Kuna watu wengi
wanatembea bila kujijua kama wamerogwa. Blog yako hii sasa imeamua kusaidia
wananchi kama hawa ili wajijue kama maisha yao yameingiliwa na mkono wa mtu. Kutokana
na roho nzuri sana ya mkuu wa blog hii , mtaalamu kutoka mkoa mmoja ambao
hautatajwa hapa kuepusha wabaya, ameajiriwa na blog na analipwa kwa fedha za
kigeni ili kusaidia kutoa ushauri
hata tiba kwa wale ambao wamejikuta wamelogwa. Kitu cha kwanza ni kujua kama
umelogwa au la, zifuatazo ni dalili za wazi kuwa maisha yako yako chini ya
mkono wa mtu. Tutakuwa tunaongeza ishara hizi kila zitakapokuwa zinatokea,
naomba nimuachie mtaalamu aeleze dalili za kujua umelogwa
Kimsingi
ukiwa na moja kati ya yafuatayo tuandikie chini kwenye comment tujue namna ya
kukushauri;
1. Ikiwa umefanya kazi katika
kampuni shirika au kwa mtu binafsi miaka kumi bila kupandishwa cheo au
kuongezwa mshahara.
2. Kama ulifeli Kiswahili na
hesabu kwenye mitihani yako
3. Kama kila ukimuona
mwanajeshi unapata hisia za kumzaba kibao
4. Kama una gari linalokuwa muda
mwingi zaidi gereji kuliko barabarani
5. Kama wewe ni mpenzi damu wa
Arsenal
6. Kama kila ukipigwa picha
unatoka hujapendeza
7. Kama mwanao wa pekee anabwia
unga
8. Panya wamekula jina lako tu
kwenye vyeti vyako vya elimu.
9. Ukijikuta unachelewa ndege
10.
Ukijikuta unanyang’anywa pointi za ligi.
11.
Unapokosea na kutumia super glue badala ya matone ya dawa ya macho.
12.
Ukijikuta unaota unatekwa.
Kwa
leo mtaalamu ametuacha hapa tukutane tena baada ya siku chache kuongezewa
dalili za kurogwa. Tafadhali tuandikie kama unaona kuna kitu kinakuhusu
Hahahahhah nimejikuta nacheka kwanguvu mpk niliokaa nao wananian
ReplyDeletegalia mm tu.
UTAKUWA ZZUZU UZEENI
ReplyDelete