Jamaa
fulani alikuwa na tabia ya kutoa ushuuz kwa nguvu kila aamkapo asubuhi. Mkewe
alikerwa sana na tabia hiyo, alimkataza akachoka, siku moja akamwonya kuwa iko
siku badala ya ushuzi, utumbo utakuja kumtoka. Jamaa alicheka sana kusikia
hilo. Siku moja mke alilazimika kuamka alfajiri awatengeze kuku kwa ajili ya
sherehe, alipowatoa utumbo wale kuku akakumbuka alichowahi kumwambia mumewe
akaamua kumtisha, akamnyatia mumewe ambaye alikuwa bado amelala na kumuwekea
utumbo kwenye pajama lake na kurudi jikoni. Muda si mrefu mwanaume aliamka akaachia
ushuzi kwa nguvu kama kawaida yake, lakini akahisi kitu cha baridi ndani ya
suruali, ile kuvuta si akakuta utumbo. Akapiga ukelele,’Mama yangu nimekufa’.
Mke wake aliposikia akacheka peke yake, akajua jamaa kashaukuta ule utumbo.
Kimya cha kama nusu saa kilipita. Hatimaye jamaa akamfuata mkewe jikoni akiwa
amelowa jasho pajama nzima.
JAMAA: Mke wangu yale uliosema
leo yametokea.
MKE: Yepi jamani?
JAMAA: Mke wangu ulisema
nikiendelea kujamba utumbo utatoka, leo utumbo si umetoka kama ulivyosema
MKE: Pole mume wangu, sasa
imekuwaje?
JAMAA: Namshukuru Mungu,
nimejitahidi nimeusindilia na vidole na nimeweza kuurudisha ndani wote.
MKE: Mungu wangu umefanyaje
wewe?
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE