Yaani Mbongo ana njia mbadala nyingi za kubadili tatizo kuwa fursa. Hizi wiki
chache zilizopita nimekuwa najitahidi kuhudhuria harusi ili nijifunze ubunifu
wa Wabongo, nakwambia si mchezo hawa jamaa waone hivi hivi. Baada ya kuingiza
kipengele cha hotuba za wazazi, ambapo wazazi husimama na kutoa hotuba ndefu
nyingine zinaboa vibaya sana nikawa najiuliza kwanini ma emsi wasifute hiki
kipengele, kinapoteza muda tu, we jitu zima linaolewa ndio unadhani hotuba za
siku ya harusi zitabadilisha tabia ya mtu? Yaani hapo ni siasa tu. Si unajua
wanasaisa wanavyohutubia mambo hata
hawayajui, we utakuta mtu akichaguliwa tu na wananchi basi anajiona anajua kila
kitu, utasikia anatoa ushauri wa kilimo, ujenzi, ufugaji, usanii kila kitu
anajua. Ene wei hao ndio kazi yao turudi harusini, niliongea na Emsi mmoja
akanambia kumbe vile vipengele ni njia mbalimbali za kupoteza muda watu
wasiombe vinywaji, hasa wale waliochanga, ni changa la macho kuonyesha shughuli
ilikuwa na vipengele vingi ili muda haukutosha.
Sasa siku
hizi kuna kipengele kipya. Maharusi siku hizi wanakuwa ndio wasanii
watumbuizaji kwenye harusi yao wenyewe. Yaani michango ikionekana imekaa vibaya
maharusi wanataarifiwa waanze mazoezi ya kucheza na kuimba ili kupunguza
gharama ya kukodi wasanii. Basi hapo utamkuta bwana harusi bizi anafanya
mazoezi kuimba na kucheza kama Ali Kiba au Daimondi, mwezi mzima maharusi
wanakaa mbele ya TV wanaangalia video za Kinaijeria za akina Davido wajifunze
namna ya kucheza, wengine ambao kidogo Kingleza kinapanda wataanza kufanya
mazoezi ya wimbo wa Endless love. Basi siku ya harusi kipengele cha wasanii
watumbuizaji wanakibeba wao wenyewe. Ile kuingia ukumbini, wanacheza nusu saa
pale mlangoni, kuimba wimbo wa pamoja nusu saa, Emsi kuwasifu kwa usanii nusu
saa, inakuja hotuba ya baba mzazi wa mume nusu saa , mama mzazi wa mke nusu
saa, ujue hapo saa nne usiku imeshaingia, chakula kinaletwa watu wanakula mpaka
saa tano, bwana na bibi harusi wanaimba tena, unasikia jamani wenye ukumbi
wameruhusu mpaka saa sita tu hivyo sherehe imeishia hapa. Milioni salasini
mliochanga ndio imeisha hivyo mjue.
No comments:
Post a Comment
SEMA USIKIKE